Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,745
11,872
Azimio la Bunge kuhusu Pendekezo la Kuridhiwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini leo Juni 10, 2023.



======

Leo Juni 10, 2023, Bunge la Tanzania linatarajia kujadili mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya DPWorld unaodaiwa kutotaja ukomo kuhusu Ushirikiano katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari zote za Baharini na Maziwa zilizopo Tanzania Bara

Mkataba umeibua maswali ambayo hayajapatiwa ufafanuzi wa kina ikiwemo thamani na muda wa uendeshaji pamoja na sababu za Tanzania kuingia mkataba na kampuni inayotajwa katika kesi za ukwepaji kodi na migogoro katika utekelezaji mikataba huku baadhi ya Nchi zikiikataa kampuni hiyo.

Je, unaufahamu kiasi gani Ushirikiano wa DP-World na Bandari?

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini, leo Juni 10, 2023

UTOAJI HUDUMA HAUJAFIKIA VIWANGO VINAVYOTAKIWA KIMATAIFA
Prof. Mbarawa amesema: "Pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, bado ufanisi katika utoaji Huduma za haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.”

“Hali ya sasa ya utendaji imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na Bandari shindani kikanda. Kwa mfano, wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es salaam ni Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban.”

"Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar umetokana na changamoto ikiwemo kukosekana kwa Mifumo ya kisasa ya TEHAMA, maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari kwa ajili ya kuhifadhia shehena, Maegesho ya Meli, mitambo ya kutosha na ya kisasa ya kuhudumia shehena ambayo ina gharama kubwa ya Uwekezaji.”

“Meli kutumia muda mrefu kupakia na kupakua shehena gatini kwa wastani wa Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1 inayokubalika Kimataifa, pamoja na Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa


MSINGI WA MKATABA HUU KUENDANA NA MIKATABA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Mkataba wa DP World kuendesha Bandari utakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za Miradi zitasitishwa au kuisha kwa muda wa Mikataba ya Nchi mwenyeji na Mikataba ya miradi

Amesema "Msingi wa Mkataba huu kuendana na Mikataba ya miradi ni kutokana na kwamba unaweka msingi unaowezesha kuingia na kutekelezwa kwa Mikataba 10 Nchini."


KAMPUNI YA DP WORLD INA UZOEFU WA KUENDESHA BANDARI BARANI AFRIKA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amesema Kampuni ya DP World ina uzoefu katika uendeshaji wa shughuli za Bandari Barani Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini

Amesema "Baadhi ya Kampuni zilizowasilisha nia ya kuwekeza Bandarini hazina wakati Kampuni ya DP World inaendesha takriban Bandari 6 Afrika na Bandari zaidi ya 30 Duniani kote kwa ufanisi mkubwa.”


DP WORLD INATAKIWA KUENDELEZA AJIRA ZA WATUMISHI WALIOPO
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema “Uwepo wa ajira za Watanzania hususani Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam ni kipaumbele kikubwa cha Serikali sio tu katika Azimio hili bali katika kila aina ya uwekezaji ambao Nchi itaufanya.”

Amesema “Ibara ya 13 ya Mkataba huu inaitaka DP World kuendeleza ajira za Watumishi wote waliopo, kuwaajiri Watanzania pamoja kuwaendeleza kitaaluma.”

TAUHIDA: KIONGOZI ANAYETAMKA KAULI ZA UBAGUZI TUNAMSHANGAA SANA

Mbunge Tauhida Gallos Nyimbo amesema “Nikimuona kiongozi anayewaongoza watu anatamka kauli ya kibaguzi tunamshangaa sana, mimi natokea Songea, mama yangu ni Mzaramu lakini ni Mbunge wa #Zanzibar.”

Ameongeza “Serikali haikatai kukosolewa, ikikosolewa inafanya uboreshaji zaidi.”


MDEE: MKATABA WA DP WORLD UMETAJA VITU KIJUMLAJUMLA
Akizungumzia mkataba wa #Tanzania na Kampuni ya #DPWorld, Mbunge #HalimaMdee amesema “Tuna nafasi ya kubadilisha baadhi ya vitu katika Mkataba huu lakini najua hatutabadilisha

Ameongeza “Kama Mkataba huu unagusa Mtwara, Tanga, Mwanza, Dar es Salaam na Kigoma kwani usizungumzwe kwa mapana yake? Tukiupitisha unaenda kuwa mkataba wa Kimataifa, chochote ambacho kimetajwa kijumlajumla kuhusu Bandari kitahusika.”


BOFYA HAPA KUSOMA: Maoni ya Kamati ya Pamoja Kuhusu Azimio la Bunge Kuridhia Makubaliano Kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali Ya Dubai Kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii Kwa Ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji Wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023

RASMI: BUNGE LAPITISHA AZIMIO LA KUUNGA MKONO MKATABA WA TANZANIA NA DP WORLD
1686419827237.png

Bunge limepitisha mkataba kuhusu Ushirikiano wa Tanzania na Kampuni ya Dubai ya DPWorld katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari zote za Baharini na Maziwa zilizopo Tanzania Bara, ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam

Sehemu ya Azimio hilo imesomeka, "kwa kuzingatia manufaa ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itayapata kutokana na Mkataba huu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa 11 na kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, linaazimia kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai Kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi katika Bandari Tanzania"

Mkataba huo uliibua maswali kutoka kwa Wananchi ikiwemo thamani na muda wa utekelezaji
 

Attachments

  • Bungeni.pdf
    341.1 KB · Views: 14
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom