Azimio la Arusha: Kwanini shule za Seminari hazikutaifishwa?

Kuna Shule za Seminary na kuna shule za Misheni (missionary schools)..
Hizi zilimilikiwa na Taasisi za kidini,ikiwemo,katoliki, Lutheran,..nk..
Shule nyingi sana za misheni zilitaifishwa(wadau wamezitaja sana)..
..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Thanks mkuu... Huyu muanzisha uzi tumsamehe saba mara sabini
 
Mkuu zipo seminari kibao tu zilitaifishwa. Ninajua tofaiti ya missionary schools na seminaries. Nimesoma katika taasisi hizo, so I can tell the difference
Kuna Shule za Seminary na kuna shule za Misheni (missionary schools)..
Hizi zilimilikiwa na Taasisi za kidini,ikiwemo,katoliki, Lutheran,..nk..
Shule nyingi sana za misheni zilitaifishwa(wadau wamezitaja sana)..
..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
St.Joseph school pale Posta Dar es salaam iliyopo karibu na kanisa katolic la st Joseph ilitaifishwa na kuitwa Forodhani secondary school! Serikali ya Tanzania ilitaifisha mashule yote ya taasisi za Kidini mpaka za Wahindu na mabudha! akutaifisha Seminary ata moja-kwani hizi sio shule kama shule za kawaida.hizi ni shule za kuandaa Makasisi/wachungaji wa makanisa na sio kuandaa vijana kwenda vyuo vikuu

St Francis College= Pugu Sec, St Andrew Sec= Minaki Sec, St Xavery= Kibasila Sec, Agha Khan Boys School= Tambaza Sec, Agha Khan Girls School= Zanaki Sec, Indian Girls School = Jangwani Sec, Indian Boys School= Azania Sec, St Joseph sec= Forodhan Sec,
 
Hizo nadhani zilikuwa zinamilkiwa na Kanisa lakini hazikuwa Seminari kama nimemwelewa mtoa mada. Kumbuka sio Kila shule zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki ni Seminari.

Zinaitwa shule za mashirika ya dini, ndiyo tofauti na shule za seminari. Shule za shirika la dini za kikatoliki zina mchanganyiko wa wanafunzi yaani wa kike na wa kiume inapobidi lakini seminari zake ni wanaume tu!
 
Wagalatia Ni waturuki....Mimi Ni mtanzania
Wakati wa zile nyaraka za Paul zinaandikwa Waturuki walikuwa bado huko Khazakhstan (central asia). Pale walikuwepo Wagiriki na ndiyo hasa walioandikiwa ile barua
 
Seminary maana yake ni kitalu. Seminary za kanisa katoliki ni kwa ajiri ya kuwaandaa mapadre wa baadae. Kwahiyo seminary zinaleaa miito ya watoto. Ndio maana kuna seminary ndogo(junior seminaries) hizi kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita, na kuna seminaries kubwa, hizi ni kwa ajiri ya masomo ya falsafa, theology ect
 
Moja ya Nguzo za Azimio la Arusha la mwaka 1967 ni kutaifisha vyanzo vyote vya Uchumi ikiwamo Mabenki, Mashirika ya Bima, Vyuo & Shule binafsi.

Swali ni kwamba kwanini Shule za Seminari hazikutaifishwa?
Tutajie majina ya shule ambazo hazikutaifishwa. Najua Umbwe ilitaifishwa.
 
Nadhani mleta Mada umeshapata baadhi ya majina ya shule zilizotaifishwa wakati wa azimio la Arusha shule Kama Nganza,Tosamaganga,pugu,Nsumba,Milambo na nyingine nyingi tu zilikuwa za kanisa katoriki.
Sasa ni zamu yake aje na hizo ambazo hazikutaifishwa. Wengine wanaongea tu, bila ya kuwa na ushahidi wowote.
 
Back
Top Bottom