MAMMAMIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 3,811
- 1,606
Angalia Azimio la Arusha, 1967.
"TUMEONEWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMENYONYWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEPUUZWA KIASI CHA KUTOSHA. UNYONGE WETU NDIO ULIOTUFANYA TUONEWE, TUNYONYWE NA KUPUUZWA. SASA TUNATAKA MAPINDUZI, MAPINDUZI YATAKAYOTUFANYA TUSIONEWE, TUSINYONYWE NA TUSIPUUZWE TENA," (AZIMIO LA ARUSHA, 1967).
Azimio hili liishia pale lilipopitishwa Azimio la Zanzibar, na tokea wakati huo, miaka 43 imepita na bado tunaendelea KUONEWA, KUNYANYASWA na KUPUUZWA. Kinachouma zaidi ni kuwa wanaotuonea, kutunyanyasa na kutupuuza si wakoloni wa Ulaya bali Watanzania wenzetu ambao tumewaamini kuwakabidhi madaraka ya dola (Ingawaje mara hii ya mwisho wamechakachachua waziwazi na wapo si kwa ridhaa ya Watanzania.
Kwa hiyo wana JF, Watanzania na wote walio na uchungu na Tanzania, tunahitaji kuwa na Azimio Jipya la Walalahoi, ambalo pamoja na mikakati mengine, litasomeka:
"TUMECHAKACHULIWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEIBIWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEPUUZWA KIASI CHA KUTOSHA. UAMINIFU WETU NDIO ULIOTUFANYA TUCHAKACHULIWE, TUIBIWE NA KUPUUZWA. SASA TUNATAKA KATIBA, KATIBA MPYA ITAKAYOTUFANYA TUSICHAKACHULIWE, TUSIIBIWE NA TUSIPUUZWE TENA," (AZIMIO LA WALALAHOI, 2010).