Azimia wakati alipotakiwa kuingia chumba cha kuchukua majibu ya HIV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azimia wakati alipotakiwa kuingia chumba cha kuchukua majibu ya HIV

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 14, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Azimia wakati alipotakiwa kuingia chumba cha kuchukua majibu ya HIV
  [​IMG]
  Friday, November 06, 2009 1:00 PM
  MWANAMKE mmoja mkazi wa Tabata, amejikuta akiwa kwenye wakati mgumu na kupelekea apoteze fahamu wakati alipotakiwa aingie kwenye chumba cha kuchukulia majibu yake ya HIV katika kliniki ya Mnazi Mmoja ya jijini Dar es Salaam.MWanamke huyo mwenye umri wa miaka 30, jina linahifadhiwa amejikuta akiwa katika hali hiyo baada ya kupata hofu kupokea majibu yake hayo ambayo ilikuwa ni lazima ayapokee mwenyewe.


  Wakizungumza na NIFAHAMISHE baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa mwanamke huyo alifika katika kliniki hiyo kwa ajili ya kuanza kliniki kwa kuwa alikuwa ni mjamzito.


  Baada ya kufika kliniki hapo na kuwauliza akina mama wenzake kama utaratibu aliosikia awali kabla hajafika hapo wa mama mjamzito kupimwa kama ni kweli ama ilikuwa ni uongo wa mitaani.


  Wenzake walimjibu kuwa ni kweli na ni lazima kwa mama mjamzito kuchukuliwa kipimo hicho na ndipo aanze kliniki na bila kufanya hivyo hataweza kuendelea na huduma za kliniki katika kituo hicho.


  Alijipa moyo a kuwaambia wenzake kwa kweli mimi mwenzenu naogopa sana kupima ukimwi ila kwa kuwa ni sheria basi nitajaribu lakini nina hofu kubwa juu ya hilo.


  Baadhi ya kina mma wenzake walimwambia kuwa ajipe moyo kwani wote tuna wasiwasi na kuchukua majibu hayo ila ni kujipa moto tu walimwambia.


  Wakati ya kuchukuliwa damu kwa akina mama hao ulifika na mmoja mmoja ambaye alikuja kwa ajili ya kuanza kliniki hapo aliitwa kwa ajili ya kuchukuliwa kipimo hicho na kila mmoja kutakiwa asubirie kwa dakika kadhaa kupewa majibu yake.


  Ilidaiwa mama huyo bado aliendelea kulala na kuwaambia wenzake kuwa hataweza kuchukua majibu hayo kwa kuwa kama atakuwa ameathirika atapoteza fahamu na kusema hajawahi kupima ila amefanya hivyo kwa kuwa ni sheria za hapo.


  Ilidaiwa majibu yalikuwa tayari na watoa ushauri nasaha walimuita mmoja mjoa wka ajili ya kuchukua majibu yake na endapo kama mama mjamzito umekutwa umeathirioka wanakupa ushauri nasaha na jinsi ya kujitunza katika hali hiyo ikiwemo na kukuelekeza jinsi ya kutumia vidonge kwa ajili ya kumzuia mtoto aliye tumboni asiweze kuathirika.


  Ilidaiwa baadhi ya kina mama wengine wliitw kuna waliokuwa salama na badhi yao wameathirika, ilidaiwa kuwa jina la mama huyo lilitajwa kwa ajili ya kuonana na nesi akachukue majibu yake, ghafla alipiga kelele na kuanguka chini na kupoteza fahamu.


  Baadhi ya akina mama na manesi waliokuwepo katika eneo hilo walimchukua na kumuingiza kwenye chumba maalum kwa ajili ya kumpa huduma maalum.


  Hata hivyo NIFAHAMISHE ilibahatika kusubiria hadi hali ya mama huyo iliporudi sawa na kufanya nae mahojiano kidogo na mama huyo kusema kuwa “ Unajua dada mimi ni muoga sana na nilijua hii hali itanitokea kwa kuwa sijawahi kupima ukimwi toka nizaliwe, ila kwa hapa wamenikamata” alisema


  Alipojaribu kuulizwa kwa nini alikuwa na hofu alisema sina hofu sana juu ya hilo huku maelezo yake yakipinda pinda na kudai ni uoga tu” mwandishi alimuacha apumnzike kwa kuwa bado alikuwa hayuko sawa


  Hata hivyo juhudi za NIFAHAMISHe kutaka kujua hatma ya majibu ya huyo dada ziligonga mwamba, kwa kuwa majibu yalikuwa yanatolewa kwa muhusika mwenyewe na si mtu mwingine, na hata ndugu yake walivyofika hapo hawakupatiwa majibu hayo na kuambiwa majibu atapatiwa mwenyewe pindi atakapokuwa tayari.

  Hiyo ni sheria iwe umeathirika ama la


  Baadhi ya akina mama walionekana kukimbia na kuacha majibu yao kwa kumuona mwenzao alikuwa katika ali hiyo, na wakilalamikia utaratibu huo uliowekwa na Wizara ya afya na kusema haufai wengine wakisema unafaa kwa kulazimishwa kupimwa.


  Matukio haya ya akina mama kukimbia na kuacha majibu yao yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika kliniki mbalimbali kwa ajili ya hofu ya kupokea majibu hayo toka utaratibu huu uanzishwe nchini kote.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Mhhnhhhh.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280

  duniani kuna mambo
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  kabisa kabisa
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Sasa ameenda mwenyewe kurudi arudishwe na watu....wapi a wapi....kama vipi mi nashauri kuondo sida kama hii waanze kufikiria kwanza kupima kabla aijanasa...wewe unamnasia predeshe jianaume la watu bila kujua procedure kazi unalo bibi....na bado
   
 6. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bora angeenda kupima ujauzito kwa wakunga wa jadi!! Hospitalini hakuna ujanja, lazima upimwe ngoma..... ebo!!
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  teh tehhh mambo haya mazito sana
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  alitakiwa amuombe mungu ampe ujasiri wa kuyapokea bila woga kwani mungu hashindwi kitu chochote.
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Nov 14, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  why threat of AIDS is like this in our African-countries? there is a problem somewhere
   
 10. T

  Tanzania Yetu Member

  #10
  Nov 14, 2009
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  This is sad! I've been working as a HIV/AIDS Counselor in London for more than 7 years. I believe people need to be well informed and prepared prior the HIV test. From what I've interpret, I have strong feelings that these individual women are not psychologically well prepared to undergo HIV test. Pre and post counseling is very crucial in order to prepare individuals.

  As a Tanzanian woman myself, a mother, social worker and counselor. I guess is about time now, I should go back to my country and help out my community.
  Please feel free to contact me should you have any question.

  Naipenda Tanzania.
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280

  Thanks much for your feelings.....come now and assist'm.....
   
Loading...