#COVID19 Azim Dewji amvaa Gwajima sakata la chanjo, amwambia ana akili ya kuhubiri siyo Sayansi

Mkuu....

Kwa hiyo unadhani hizo chanjo zimeingia nchini na kuidhinishwa bila ya kufanyiwa tafiti?!!!

Je hakukuwa na SAMPLE iliyotumwa hapa nchini miezi kadhaa nyuma na kufuata mlolongo wa KUANGALIWA....Wataalamu wanajua....labda walimfanyia SOKWE.....

Nina imani serikali yetu adhimu haikukurupuka Kwani si mara ya kwanza KUPIMA UBORA WA CHANJO TOFAUTI.....
Kama wao hiyo johnson & jonosn wameikataa leo wewe ndo unaiona ni bora!!!! Kwa maabara gani ulizonazo acheni kujitoa ufahamu
 
Gwajima anapaswa kujibiwa kwa hoja

1) Anataka tuambiwe ni daktari yupi Tanzania amefanya thorough analysis ya kilichomo kwenye hiyo chanjo?

2) Tuambiwe chemical composition ya contents za hizo vaccine

3) Tuambiwe kama kuna/hakuna potetial side effects za hiyo vaccine leo, kesho, 30 years later

4) Tuambiwe chanjo wanayopewa wamarekani ndiyo hiyohiyo tunatakiwa kupewa sisi? Kwa mfano, kwanini tumepewa Johnson & Johnson wakati wao wanatumia zaidi AstraZeneca?!

Naona wengi wanatukana tu na kusema eti “ amuheshinu Rais na mwenyekiti”. Akili za kitumwa hizi.
 
Mbunge ana madaraka ya kusema alichosema, yeye ana position ipi kusemea Covid-19 kuwaambia watu wasichome. Who is he? Mkuu wa nchi kashalisema vema sana kuhusu Covid-19. Ni hiari yako kuchanja, sasa Gwajima anatisha watu who is he? Ni kumfukuza huyu CCM haraka sana.
Mbunge "ana" au "hana"?
 
Watanzania wengi ni vilaza, Inamaana wameshindwa kabisa kujibu hoja za Gwajima na badala yake wanamtusi na kufosi bila kutia majibu ya maswali yake

Bahati nzuri kasema vita hii ataipiga hata akibaki peke yake
 
Azim Dewji: Tunasema kwamba, kazi kubwa ya mkuu wa Dini ni kuongoza waumini wake sio kuwapotosha, unazungumza maneno ya kuwapotosha waumini na kuleta taharuki kwenye Jamii, hiyo haifai kabisa na isiendelee kufanyika hivyo, sisi hatutakubali.

Kwa njia moja au nyingine unawatukana waliobobea kwenye fani hiyo kwamba kamati iliundwa, waliofanya utafiti wewe unawaona hawana akili. Saa nyingine naweza kusema labda wewe ndio huna akili ya sayansi, wewe labda una akili ya kuhubiri peke yake kwa hiyo usijaribu kuwatukana wenzako.

Mwisho Azim amemwambia mchungaji Gwajima amuheshimu Rais na kiongozi wa chama ambacho kimemlea na kumpatia ubunge kwani bila chama cha CCM asingepata ubunge na wengine kama yeye hajampigia kura Gwajima bali alipigia chama.

PIA, Soma> Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

hivi hawa wahindi wamezaliwa hapa, wameishi hadi wamezeeka lakini hawajui kiswahili vizuri huwa sababu yake nini, au wanajifanyisha?
 
Inashangaza kumuona mbunge anaongea maneno yale....

Yaani wakitokea MANESI na MADAKTARI wetu wanahimizana kuchanjwa chanjo dhidi ya UVIKO....wanatuhimiza Raia dhidi ya chanjo hiyo basi GWAJIMA amewaombea WAFE...WAFARIKI DUNIA...."WAKUFE" Khaaa

Waziri wa afya ,mh.Dr.D.Gwajima ni DAKTARI KWA TAALUMA .....

Katibu mkuu Wizara ya Afya ni DAKTARI KWA TAALUMA....

Binafsi nimeshangazwa na kusikitishwa sana na kauli ya ndugu Askofu Gwajima......

It's really terrible...

Terrible....
Terrible....

#TujiandaeKuchanjwaChanjoHiyo
#AfyaZetuNiMuhimu
#NchiKwanza
#JMTMilele
#KaziInaendelea
Hao uliowataja wote siwezi kuwaamin,wakat wa jiwe walituambia corona hakuna,na pia wakatusihi tupige nyungu kwasana,Leo wanatuambia NINI?
 
Boss, ukizungumzia wataalamu na nchi yetu, basi sahau kabisa kuhusu huo utalaamu wenyewe.

Sisi tuzungumzie 10% na upigaji usio na aibu, dhuluma na husda, uzandiki na unafiki, umelo na ulafi, majivuno na majigambo, ubabe na uhafidhina, uzuzu na umbumbumbu na yote yafananayo na tunayofanya.

Utaalamu? Upi? Sayansi? Ipi? Angalau tunao uwezo kwa kukariri na kukumbuka historia ya sayansi, kubeba ya watu kichwani na kufanya ni yetu!

Huna utaratibu maalum wa kupima watu, huna takwimu zozote za jambo hili, unasema kuna wagonjwa 680 wa covid-19! Sina hakika kama wenzetu wanazungumzia mamia tena, ina maana hatukua na rekodi kabla, sio? Wangapi wamekufa kwa covid-19 mpaka sasa? Wangapi wamepona? Wangapi wako ICU, tupe taarifa hata ya kupika tu ili tujue tuko wapi!

Imeundwa kamati, miezi 4 mbele unaliambia taifa kwa kusisitiza, mimi ni waziri wenu, hali ni mbaya! Kuna siri gani ya kutosema kwa namba ubaya wa hali hiyo? Kama chanjo zishafika, nini kingine tunaogopa? Kama ni JPM, hayupo tena, kigugumizi kinatoka wapi?

Ubavu wa kutoa matokeo ya kusema wewe ni COVID-19 positive huna, kwamba usipopewa cheti wewe ni mgonjwa au eti unatoa majibu NOT NEGATIVE, mtu huyo akirudia ndani ya siku 5 bila kinga wala isolation unampa cheti kuwa NEGATIVE, na bado unataka tuamini kuwa unajua unachokifanya? Unipime kwa takribani sh 400,000, ambapo dola 100 za serikali na pesa kadhaa za kituo, halafu unipe chanjo bure? Na bado zikipita saa 72 cheti ni invalid, biashara iliyoje hii.

Huruhusiwi kupanda daladala bila barakoa na yote waliotangaza, ila kundi la wanafunzi shuleni wanaokaa 90 kwa chumba kimoja cha darasa hawajazungumzwa itakuaje! Barakoa zibadilishwe kila baada ya saa 4, sijui kama kule Nanjilinji wataweza. Wataalamu walioshindwa kuthibitisha kama barakoa tulizonazo, ama za vitambaa au zile za hospitali kama zinaweza kuzuia mdudu kupita! Vyuoni huko wanaweza kukaa mita 1 apart?

Nchi ina wagonjwa wangapi wa njaa? Malaria? Watuambie hapa kwetu, ni ugonjwa gani uko kwa wingi na unaongoza kwa kuua, ili tujue tahadhari zaidi zielekezwe wapi!

Tumepitisha bajeti juzi, tumesema tunaongeza tozo kujenga barabara na zahanati, kama tungejali sana, tungetenga fedha za kununua hivyo vifaa vya kusaidia upumuaji na kuongeza ICU facilities kwa dharura, mpaka sasa tumeongeza ngapi? Uliza wakurugenzi wangapi wanapewa pesa za magari mapya kama yamekosekana kabisa ya kuwabeba! Majumba mangapi ya ma RC na DCs yanajengwa/karabatiwa kwa mafedha chungu mzima kwa mujibu wa bajeti, lakini tuna uhaba wa mashine za kusapoti upumuaji?

Jokate anaweka taa mbele ya ofisi yake kwa mamilioni ya fedha, Temeke hospitali tuna mitungi mingapi ya gesi ikitokea kweli kitu kimelipuka?

Sipingi chochote mkuu ILA najaribu kuomba kama kweli kuna dharula, basi tufanye vitu umuhimu wa dharula hiyo na sio hata wasio na mamlaka ya kusema wanasema tu.
Umeandika kwa hisia kali sana, wakijibu haya maswali itapendeza!!
 
wana standard zao na viwango vyao ambavyo ni tofauti na sisi yaani una pesa ya kuinunua kumbuka ni dunia ya kwanza vs dunia ya tatu acha kutumia nguvu nyingi sana kwa jambo ambalo ni dhahiri kabisa,kumbuka tu kuwa mzungu angekuwa anahitaji hilo la kuiangamiza Africa wala asingesubiri covid na asingefanya hadharani kama picha zako zinavyomaanisha.Na ndio maana hata dawa za ukimwi hizi zinazoletwa africa unadhani ndizo wanazotumia US au CANADA au EU ni tofauti kabisa.(standards)
 
Yeye Azim Dewji ni Mwanasayansi?

Azim Dewji: Tunasema kwamba, kazi kubwa ya mkuu wa Dini ni kuongoza waumini wake sio kuwapotosha, unazungumza maneno ya kuwapotosha waumini na kuleta taharuki kwenye Jamii, hiyo haifai kabisa na isiendelee kufanyika hivyo, sisi hatutakubali.

Kwa njia moja au nyingine unawatukana waliobobea kwenye fani hiyo kwamba kamati iliundwa, waliofanya utafiti wewe unawaona hawana akili. Saa nyingine naweza kusema labda wewe ndio huna akili ya sayansi, wewe labda una akili ya kuhubiri peke yake kwa hiyo usijaribu kuwatukana wenzako.

Mwisho Azim amemwambia mchungaji Gwajima amuheshimu Rais na kiongozi wa chama ambacho kimemlea na kumpatia ubunge kwani bila chama cha CCM asingepata ubunge na wengine kama yeye hajampigia kura Gwajima bali alipigia chama.

PIA, Soma> Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Mbunge hana madaraka ya kusema alichosema, yeye ana position ipi kusemea Covid-19 kuwaambia watu wasichome. Who is he? Mkuu wa nchi kashalisema vema sana kuhusu Covid-19. Ni hiari yako kuchanja, sasa Gwajima anatisha watu who is he? Ni kumfukuza huyu CCM haraka sana.
Wewe nenda kachanje chanjo hakuna aliekuzuia na wale ambao hawatataka kuchanjwa acha waendelee kukataa, swala la watu kumsikiliza Gwajima na kukataa kuchanjwa lipo ndani ya utashi wao hivyo usiwapangie.

Kwani sio nyinyi mnaodai freedom of speech kila siku humu?
 
wana standard zao na viwango vyao ambavyo ni tofauti na sisi yaani una pesa ya kuinunua kumbuka ni dunia ya kwanza vs dunia ya tatu acha kutumia nguvu nyingi sana kwa jambo ambalo ni dhahiri kabisa,kumbuka tu kuwa mzungu angekuwa anahitaji hilo la kuiangamiza Africa wala asingesubiri covid na asingefanya hadharani kama picha zako zinavyomaanisha.Na ndio maana hata dawa za ukimwi hizi zinazoletwa africa unadhani ndizo wanazotumia US au CANADA au EU ni tofauti kabisa.(standards)
Mkuu kwani Gwajima kakukingia bunduki Ili isiende kuchanjwa? Wewe nenda kachanjwe wale wasiotaka kuchanjwa baada ya kuskiliza Gwajima achana nao Ili kama ni kufa kwa COVID-19, basi wafe.

Kachanjwe mkuu.
 
Kuchanja ni hiyari na Gwaji kama mchungaji mwacheni awaambiye kondoo zake wasichanjwe kwani wakidhurika atakosa sadaka. Na hizi sheria mpya zitamnyima kufanya mikusanyiko ndiyo maana anazipigia kelele, akikosa watu amekosa sadaka. Mwacheni azungumze anayoyafikiria ni sawa. Tupo huru kusema tunayoyaona ni sawa.
mkuu uhuru usio na mipaka si rahisi ila la msingi asingeamua kumtumikia Mungu na Kaisari kwa wakati mmoja haijarishi yuko wapi yeye ni Mbunge wa ccm achunge ulimi wake hayo maneno aliyoyasema sio sawa,ni muda tu ila anaweza kuitwa kuhojiwa na wenye chama.
 
Huko nyuma tuliambiwa tusichanganye dini na siasa, lakini sasa ndiyo ninajua huo msemo ulikuwa na maana gani. Ikiwa itaonekana alichokisema ni kosa na chama chake basi hata wakimwita itakuwa ni sawa tu kwani hayo ndiyo matunda yao wenyewe waliyoyavuna katika uchaguzi uliyopita.
Removing of force from oppositions creates opposition force from within.
 
Azim Dewji: Tunasema kwamba, kazi kubwa ya mkuu wa Dini ni kuongoza waumini wake sio kuwapotosha, unazungumza maneno ya kuwapotosha waumini na kuleta taharuki kwenye Jamii, hiyo haifai kabisa na isiendelee kufanyika hivyo, sisi hatutakubali.

Kwa njia moja au nyingine unawatukana waliobobea kwenye fani hiyo kwamba kamati iliundwa, waliofanya utafiti wewe unawaona hawana akili. Saa nyingine naweza kusema labda wewe ndio huna akili ya sayansi, wewe labda una akili ya kuhubiri peke yake kwa hiyo usijaribu kuwatukana wenzako.

Mwisho Azim amemwambia mchungaji Gwajima amuheshimu Rais na kiongozi wa chama ambacho kimemlea na kumpatia ubunge kwani bila chama cha CCM asingepata ubunge na wengine kama yeye hajampigia kura Gwajima bali alipigia chama.

PIA, Soma> Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Dikteta Mwendazake ndio amesababisha Nchi imekuwa na watu wapuuzi na wahuni kama Gwajima Ku address Taifa
 
Back
Top Bottom