AzamTV mnashindwa kuweka huduma kwa wateja Weekend?

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,372
Kwanza niwapongeze Azam Tv kwa juhudi zenu za kutuletea matangazo yenye ubora.

Jumapili iliyopita nilipata tatizo la kuchelewa kurudi channel baada ya kulipia kifurushi cha Azam tv.

Sasa nilipoamua kupiga huduma kwa wateja kupita namba 0784108000 kwa mshangao niliambiwa huduma hii haipatikani Siku za weekend.

1.Hivi kweli Azam Tv mnashindwa kuweka huduma kwa wateja kwa Siku za weekend au mmeamua tu kutowajali wateja wenu?

Inawezekanaje nipate tatizo la dharura jumamosi inilazimu kusubiri mpaka Jumatatu?

2.Pia imarisheni ubora wa rimoti zenu maana vitufe vinawahi mno kuharibika hasa kile cha katikati "OK",hii nayo ni kero

Jirekebisheni kama kweli mnataka kuendana na kaulimbiu yenu ya 'burudani kwa wote"

Kero zangu ni hizo kwa leo.

Ahsante.

IMG_20191024_121537.jpeg
 
Mimi nawapongeza kwa kutuwekea channel mpya za dini ikiwemo hii ya Upendo Tv! Ushauri wangu kama upo uwezekano, watuwekee na ile ya Wakatoliki (Tv Tumaini). Hakika mambo yatakuwa bambam.
 
Upendo TV ni ya dhehebu gani?
Mimi nawapongeza kwa kutuwekea channel mpya za dini ikiwemo hii ya Upendo Tv! Ushauri wangu kama upo uwezekano, watuwekee na ile ya Wakatoliki (Tv Tumaini). Hakika mambo yatakuwa bambam.
 
Azam TV.
Kila Jumapili Emmanuel TV inakosa sauti kwenye Ibada ya moja kwa moja.
Kulikoni inatokea Jumapili tu kwenye Ibada Live ?
 
Naam Mkuu,,, hiyo changamoto ipo na wanasahau kuwa siku zite wanakuwa hewani(kwa maana ya Huduma ya matangazo).In addition niwashauri watumie namba maalumu ambayo ni free kuliko hivi tunakatwa salio wakati sisi ni Wateja wao ,,,,,tunawachangia vifurushi kila mwezi.
 
Tanzania kampuni ambayo ipo makini huduma kwa Wateja ni Dstv tu... Muda wote unasikilizwa wakati mwingine wanakupigia simu wenyewe.

Kwa mbali wanafuatia Vodacom.!
 
Ni kweli mkuu
 
Tanzania kampuni ambayo ipo makini huduma kwa Wateja ni Dstv tu... Muda wote unasikilizwa wakati mwingine wanakupigia simu wenyewe.

Kwa mbali wanafuatia Vodacom.!
Aisee,ila tatizo bei za vifurushi zipo juu
 
Back
Top Bottom