Azama FC Yaadhiriwa na "Dogo Dogo" Zanzibar. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azama FC Yaadhiriwa na "Dogo Dogo" Zanzibar.

Discussion in 'Sports' started by Junius, Aug 12, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  TIMU ya soka ya Azam FC kutoka jijini Dar es Salam iliopo visiwani humu kwa ajili mazoezi yake ya mwisho imeangwa rasmi na vijana wa timu ya ‘Zanzibar Heroes’ kwa kuchapwa bao 1-0 bila ya huruma.
  Katika pambano hilo ambalo lililofanyika katika dimba la uwajua wa Mautsetung Mjini Unguja, timu ya Azam iliweza kumilikiwa vyema na vijana wa Zanzibar katika dakika zote za mchezo.
  Mchezo huo ulianza vyema huku mashabiki wa timu hizo wakioneka kuwa na furaha kubwa katika nyuso zao huku uwanja ukijaa mashabiki wakiwa na hamu ya kuona hali ya ngarambe hizo za mwisho kwa timu ya Azam.
  Mara tu ya mchezo huo kuanza vijana wa Zanzibar waliweza kuutia mpira miguuni mwao na kufanikiwa kuliona lango la Azam FC na kuanza kuzitikisha nyavu zao, kupitia mchezaji wake Hassan Seif ‘Banda’ mnamo dakika ya pili ya mchezo huo.
  Bao hilo ambalo liliwafanya Azam kutoamini macho yao kwa vijana hao kwa kuwaona ni wadogo kwa maungo lakini ndani ya miguu yao mmejaa kila aina ya madaha ya mchezo.
  Mchezo huo uliendelea hadi dakika 45, za kipindi cha kwanza vijana wa Zanzibar wakiongoza kwa bao moja bila ya majibu dhidi ya wenzao timu ya Azam ya jijini Dar es Salaam.
  Hata hivyo muda wa kipindi cha pili ulianza na kumaliza kwa timu zote mbili kutotikishiana nyavu hadi tamati ya dakika 90 za mchezo huo wa kirafiki, ambapo timu ya Zanzibar Herous ikitoka kiwanjani hapo ikiwa kifua mbele kwa bao moja kwa mzunguko.
  Mechi hiyo ya timu ya Azam FC ilikuwa ni ya tatu kucheza visiwani humu, ambapo mechi yao ya kwanza walicheza na vijana wa ‘Karume Boys’ na kufanikiwa kupata mabao 3-0, ambapo mechi ya pili walicheza na klabu bingwa ya Zanzibar timu ya Mafunzo ambayo walitandikwa mabao 2-0 mechi zote hizo zilichezwa katika uwanja wa Mautsetung Mjini Unguja na kuhudhuriwa na mashabiki wengi wa soka.

  SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
Loading...