Azam yawinda nyota wa Mbeya City na Prisons


K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Messages
1,691
Likes
2,208
Points
280
K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2013
1,691 2,208 280
azam-jpg.630104

Keshokutwa Jumatano dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufunguliwa, tayari nyota wawili wa Mbeya City na Prisons wamekuwa kipaumbele kwa Kocha wa Azam FC, Mromania, Aristica Cioaba.

Nyota hao ni Mohammed Rashid wa Prisons ambaye mpaka sasa ana mabao sita, pamoja na Eliud Ambokile wa Mbeya City mwenye mabao manne.

Wawili hao wameonekana wanaweza kutibu tatizo la ushambuliaji linaloisumbua timu hiyo.
Hivi karibuni, Azam iliachana na straika wake Mghana, Yahaya Mohammed, huku Aristica akitangaza kuingia sokoni na kuchukua mastraika wawili wazawa ambao anaamini watalitatua tatizo hilo linalowasumbua tangu kuanza kwa msimu huu.

Mmoja wa watu wa benchi la ufundi la timu hiyo, ameliambia Championi Jumatatu: “Majina ya Mohammed Rashid na Eliud Ambokile yamekuwa ya kwanza kutajwa na kocha kwani anadai amewafuatilia kwa umakini na kubaini kwamba wanamfaa katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

“Kinachosubiriwa ni kamati ya usajili ikae iweze kuangalia uwezekano wa kuwasajili kutokana na mapendekezo hayo ya mwalimu.”

Alipotafutwa Meneja wa Azam FC, Philipo Alando, kuzungumzia masuala ya usajili ndani ya timu hiyo, alisema: “Baada ya mechi yetu ijayo ndiyo kamati itakaa kujadili ripoti ya kocha ili kuona nani anahitajika kusajiliwa kwa sababu kuna sehemu zinaonekana wazi kabisa bado zina upungufu.”

Salehe Jembe
 

Forum statistics

Threads 1,251,183
Members 481,615
Posts 29,761,523