Azam yatua EPL

Mkuu ukifanya comparison ni vizuri kuweka kwa currency moja. Ila nashukuru kwa hiyo info, siyo mbaya ukanielekeza ulipo pata hizo taarifa.
 
 
Kama alivosema Root Multichoce wametoa hela ndefu sana . Hii ni ya msimu wa 16-19


Msimu wa 19-22 ambao walirenew mwaka jana tunategemea hela itakua ndefu zaidi ya hiyo. Sasa ukilinganisha na Azam ambao uwezekaji wao wote nasikia ni sh.50 billion huoni kama ni mbingu na ardhi mkuu?
Aliye kwambia amekudanganya studio peke yake walitumia zaidi ya bilioni 40, Kandarasi alipewa mwingereza.
 
Kawaida sana siku za nyuma Star Tv waliwahi kuonesha, karibuni Tv1 na Eatv walikua wanaonesha so sioni jipya kwakua bado wameangukia kwa walichokua wakifanya wenzao
 
Kuweka rekodi sawa, Dstv hawaonyeshi Bundesliga na King'amuzi chao kwasasa ni 99,000/=
Ni elfu 70 tu boss tena hadi gharama za ufundi, nafanya hizi kazi za kuvifunga mahala nakoishi.
.
Changu sijakilipia miezi minne sasa nadhani ni 209,210 inaonyesha Bundesliga ila i'm not so sure
 
Mbona wametoa matangazo UTV mpira ulipotaka kuanza tu?kama kuna mashart ili mtu uone mechi wangetuambia sasa niko home hata namna ya kutoka kuangalia game vibandani nashindwa
 
Azam wanazidi kupoteza credibility kwa wateja..yaleyale ya AFCON..
 
Sio kwamba Azam ni threat kwa DSTV haiwezekani kabisaa.Kwa mtaji walionao DSTV hata wakigawa bure kabisa madish yao na decoder kisha watu wakaanza kulipia vifurushi vyao bado wanaweza kujiendesha.Azam wanajitahidi lakin bado sana kufananisha au hata kuikaribia DSTV.Hata wenye madish yote mawili mara nyingi hupenda kuwasha DSTV.Azam inawashwa saa2 usiku kwenye habari na siku za VPL.Baada ya hapo unafunga.

Mteja wa DStv akilipia 19,000 kwa mwezi channel anazopewa ni pungufu kidogo tu kwa package kubwa ya Azam.Sasaivi Dstv(multichoice)wameshabalance mzani wa soko kwa hiyo ndo maana wanajiamini hata kupunguza vifurushi vyao na bando kampuni haiyumbi.Ni sawa na supersport ambao sasaivi hakuna mtangazaji mkubwa kuliko kituo.Hata baada ya kuondoka yule wa uefa(sikazwe)kama sijakosea bado Supersport ipo vizuri na haiwezi kuyumba.
Hata hivyo azam wapo vizuri ila wapambane kwanza na startimes maana ndo mshindani wao mkubwa sana.
Star times wameng'oa Fox zote mbili yaani kumuona samatta tena mtihani.Ligi za Uholanzi,Belgium na ile ya kwa Trump zilinifanya binafsi nikasahau kabisa habari za Ligi ya uingereza.Sijawaelewa kwa kweli.Kuwauliza wanatoa majibu ya mkato mkato tu.
 
Star times wameng'oa Fox zote mbili yaani kumuona samatta tena mtihani.Ligi za Uholanzi,Belgium na ile ya kwa Trump zilinifanya binafsi nikasahau kabisa habari za Ligi ya uingereza.Sijawaelewa kwa kweli.Kuwauliza wanatoa majibu ya mkato mkato tu.
Tafuta espn ndiyo zimebadilisha jina na kuitwa hivyo.
 
Back
Top Bottom