kidadari
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 8,647
- 9,573
Baada ya Azam media kuonyesha mechi chache za ligu kuu bara msimu uliopita ambapo Azam wana haki ya kuonyesha mechi hizo. Wadau wa michezo wakawataka TFF kuwabana Azam ili watimize vigezo vya kuonyesha walau 90 % ya michezo yote itakayochezwa.
Wadau wa michezo walitegemea Azam media kuongeza channel nyingine au kufanya mabadikiko ya vipindi vyake ili kuonyesha mechi hizo lakini cha ajabu katika kikao cha TFF na Azam Media waliwaruhusu azam kupanga ratiba mechi zianze saa 8 badala ya saa 10 kama hapo awali.
Jambo hilo likipingwa na timu pamoja na wachezaji kutokana na hali ya hewa maeneo mengi kuna jua kali na joto kali linalowaathiri wachezaji ,pia si muda rafiki kwa mashabiki kuingia uwanjani wengi wao bado wapo makazini lakini TFF walishupaza shingo na kuruhusu maamuzi hayo.
Soka la Bongo.