Azam TV yakanusha kukwepa kodi ya ongezeko la thamani(VAT)

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Azam PayTV Ltd ya Mauritius ndiyo mmiliki wa Azam Tv inayoonekana katika nchi zote za Afrika Mashariki na Kati pamoja na nchi nyingi za kusini mwa jangwa Ia Sahara kwa njia ya Satelite. Kampuni hii inawakilishwa na Azam Media Limited hapa nchini Tanzania.

Azam Media Limited inapenda kuufahamisha Umma kuwa;

  1. Taari fa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa AZAM TV inakwcpa kulipa kodi ya Ongezcko la thamani (VAT) si kwcli na zinakusudia kuupotosha umma kwa ujumla.
  2. Tozo ya hudurna za Azam tv inalipiwa kodi ya Ongezeko Ia Thamani (VAT) kwani mmiliki wake arnbayc ni Azam Paytv Ltd ya Mauritius amcsajiliwa hapa nchini kwa madhumuni ya ulipaji wa kodi ya Onge-teko Ia Thaman i (VAT) kwa usajili nambari VRN 40-023191-C
  3. ldadi ya watcja Milioni 3 waliofungiwa ving'amuzi vya Azam TV iliyoripotiwa katika mitandao ya kijamii si ya kweli.
  4. Azam TV inatoa rai kwa wctcja wake na wananchi kwa ujumla kupuuza taarifa za uzushi na uongo zenyc lengo Ia kuchafua jina Ia Azam TV na kurudisha nyuma juhudi za Kampuni kutoa huduma bora ya Runinga kwa watcja wake
  5. Pia Umma unatahadharishwa kuwa makini na taarifa mbalimbali zinazosambazwa katika rnitandao ya kijamii mara kwa mara kuhusu AZAM kwani taarifa hizo zina malcngo ya kuchafua jina Ia AZAM arnbalo linakubalika hapa nchini na nchi zotc barani Afrika.

Hussein Sufiani
Mkurugenzi wa Mawasiliano
12 JULY 2016


Azam.jpg
 
TOA MCHANGANUO WA NAMNA VAT ILIVYOLIPWA , MAELEZO YAKO MAFUPI MNO

Nimeweka kama nilivyopokea mkuu, Lakini VAT ya jana itakua sio hiyo tena kwa sababu idadi ya waliofungiwa ving'amuzi imebadilika.
 
Nimeweka kama nilivyopokea mkuu, Lakini VAT ya jana itakua sio hiyo tena kwa sababu idadi ya waliofungiwa ving'amuzi imebadilika.

MKABILI MTOA TAARIFA AKUPE IDADI KAMILI YA WATEJA WAKE, MAKUNDI YAO NA TOZO KWA KILA KUNDI ILI TUKOKOTOE VAT KWA MAENDELEO YA INCHI
 
Ukute huyu jamaa aliyeandika hao ni Afisa habari mwandamizi wa Azam? Bora ungekaa kimya maana" badala ya kuling'oa umelishindilia" Wenzangu wa Bukoba wanelewa namaanisha nini.
 
Sijaona ufafanuzi wowote ule kutoka Azam PayTv toka Mauritius.

Badala ya kuelezea jinsi wanavyolipa hiyo kodi, wanatuwekea TIN Namba....hiyo Tin mbona kila mtu anayo?

Ufafanuzi upi zaidi unaoutaka? Wamejibu kuwa wanalipa kodi na TIN namba yao wamekuwekea na pia wamesema kuwa wateja millioni tatu ni uongo.

Sasa unataka nini zaidi?
 
TOA MCHANGANUO WA NAMNA VAT ILIVYOLIPWA , MAELEZO YAKO MAFUPI MNO

Kampuni ya Mtanzania inasajiliwa Mauritius ili ifanye kazi Tanzania kwa sababu zipi za msingi - kwani wakati inafunguliwa huko ina maana taasisi nzima ya BRELA ya hapa nchini ilikuwa imekwenda likizo hivyo kulazimika kwenda in one of Indian Ocean Islet kufungua kampuni?

Dunia nzima inajua kwamba ukiona raia wako anasajili kampuni yake nje ya nchi alafu ifanye biashara ndani ya nchi - basi jiulize maswali mengi: kubwa likiwa ni kitu gani anataka kisijulikane au kisifatiliwe kwa karibuni.

Kitu kingeni, kwa nini mleta mada anajibu maswali kijuu juu tu kwa nini aleti takwimu zake tukazilinganisha na zile zilizo tolewa na a whistleblower - hii ingesaidia sana members kubaini nani mkweli na nani mzushi.

Allegation hizi ni serious Management ya AZAM isichukulie lightly.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom