Azam TV yafuta post zake haraka zilikuwa zikiimuonyesha Tundu Lissu akichukua fomu za Urais NEC Dodoma

Wasiojulikana watajulikana tu. Subiri dozi iendelee.

Lawama kwa yule kijana aliyeshindwa kumuua mnyaturu kwa risasi zaidi ya 30.

Mzimu umefufuka, wasiojulikana hawajui waanzie wapi.

Ushauri: CCM endeleeni na shughuli zenu muacheni Lisu afanye yake. Akishinda urais tume ni yenu, mtajitangaza tu wala hakuna wa kubisha. Tume, polisi, TISS, JWTZ wote wapo upande wenu. Mlichokosa ni uhalali tu wa kuongoza kutoka kwa wananchi.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
Sawa kabisa. Watulie bila wasiwasi.
 
Wakuu habari,
Katika hali ya kushangaza azam tv kwenye kurasa zake za mitandao mbalimbali waliweka video zikimuonyesha Lissu akichukua fomu za kuwania urais kweny ofis za Nec huko Dodoma lakini muda mchache wakazifuta hizo post zote,hii inaashiria nini kwenye tasnia hii ya habari?
Hapa ndipo jiwe alipolifisha Taifa letu pendwa, kwake siasa ni uadui
 
Anandika

na malisa

Nimekuwa nikisoma kwenye vitabu na sasa nashuhudia kwa macho. Uhuru wa habari unakanyagwa na watu hawathubutu kukemea kwa sababu ya HOFU. Vyombo vya habari vilivyoalikwa kuripoti tukio la Lissu kuchukua fomu havijatokea kwa sababu ya HOFU.

Azam wakavuka kiunzi cha HOFU na kwenda kuripoti. Lakini ghafla wakakatisha matangazo na kufuta post zote zinazohusu Lissu kuchukua fomu. Nimeshangaa sana.

Kuna watu wanashangilia kuona uhuru wa habari ukiminywa ili wafurahishe mamlaka. Na wengine wanaogopa kukemea ili nao wasiingie kwenye makucha ya mamlaka. Tukifika hapa hakuna aliye salama.

Jana @advocate_jebra alieleza kisa cha Simba na Kondoo. Simba alifungiwa kwenye kizimba kwa siku kadhaa. Akawa anatafuta msaada wa kufunguliwa kwa nje. Kondoo akapita. Simba akamwambia nifungulie naahidi sitakula. Kondoo akamwambia Simba apa, akaapa. Kondoo akamfungulia.

Alipotoka akamrarua kondoo na kutaka kumla maana alikua na njaa ya siku kadhaa alizofungiwa kwenye kizimba. Wanyama wengine wakapita wakakuta Simba na Kondoo wakizozana. Kondoo akajielezea, Simba nae akajielezea. Simba akakiri ni kweli aliahidi hatamla kondoo lakini ana njaa ya siku 3 afanyeje?

Wanyama wote kwa sababu ya HOFU wakaunga mkono maelezo ya Simba kuwa amle tu kondoo, maana alikua na njaa.

Kobe akasema hajaelewa mkasa huo vizuri. Akamuuliza Simba unasema ulifungiwa kwenye kizimba? Simba akajibu ndio. Akamuuliza kipi? Akamwambia kile pale? Akamuuliza mbona kidogo sana? Uliwezaje kukaa humo? Simba akasema nilikuwemo. Kobe akamwambia hebu ingia tuone kama kweli uliweza kuenea humo. Simba akaingia, kobe akafunga komeo kwa nje na kuondoka.

Kobe akawaambia wanyama wenzie. Leo Simba angemla kondoo mngejiona mko salama kwa sababu si nyie mmeliwa. Lakini kesho angepata njaa tena, na hatujui ingekua zamu ya nani.

Ukiogopa kukemea uonevu haimaanishi kwamba upo salama. Inamaanisha umejiweka kwenye hatari zaidi. Leo vyombo vyote vimeungana na mamlaka kuzuia habari za Lissu. Nilipoona Azam wamerusha matangazo nikasema angalau tumempata Kobe wa kuokoa wenzie. Mara ghafla kobe huyo nae akaungana na wenzie kumtetea Simba amle kondoo. Bila kujua kesho Simba atapata njaa tena na hawajui itakua zamu ya nani. #Subhanallah
 
Wakuu habari,
Katika hali ya kushangaza azam tv kwenye kurasa zake za mitandao mbalimbali waliweka video zikimuonyesha Lissu akichukua fomu za kuwania urais kweny ofis za Nec huko Dodoma lakini muda mchache wakazifuta hizo post zote,hii inaashiria nini kwenye tasnia hii ya habari?
polepole kishapiga simu,
Hata milard ayo anahofu kuposti, watu wana hofu kuliko ile ya wagandda dhidi ya IDD amin
 
Wakuu habari,
Katika hali ya kushangaza azam tv kwenye kurasa zake za mitandao mbalimbali waliweka video zikimuonyesha Lissu akichukua fomu za kuwania urais kweny ofis za Nec huko Dodoma lakini muda mchache wakazifuta hizo post zote,hii inaashiria nini kwenye tasnia hii ya habari?
Yeye mwenyewe kawachokoza kwamba wasijezima tv wakati anaongea, sasa wanamjibu kabla.
 
Watanzania msihofu. Haya yote yanaashiria na kumaanisha Kuwa saa ya ukombozi ndo hii.

Nilisema kwenye uzi wangu humu. Fitna hizi zinazofanywa dhidi ya Lissu mchana kweupe na Watanzania wote tukiziona si tu zinaongeza mapenzi kwa Lissu Ila zinazidi kuwapa sababu lukuki watanzania wote wapenda haki na usawa kuwa ni lazima Magufuli atoke madarakani mwaka huu kwa sanduku la kura ili watanzania wawe huru.

Waachane tu wafanye udhalimu wao ila wakati utafika kila mtu atahesabiwa.

Lissu yupo na Mungu. Aliyemponya kwenye risasi 16 huku akiiacha risasi 1 mwilini kwake na anazidi kumpa uhai ni mkubwa kuliko vyombo vya habari uchwara vya Tanzania

Mungu wenu wa 2015 kama ni yule yule mliyesema alimleta EL awe raisi anayesubiri kuapishwa basi endeleeni kubwabwaja
 
Wakuu habari,
Katika hali ya kushangaza azam tv kwenye kurasa zake za mitandao mbalimbali waliweka video zikimuonyesha Lissu akichukua fomu za kuwania urais kweny ofis za Nec huko Dodoma lakini muda mchache wakazifuta hizo post zote,hii inaashiria nini kwenye tasnia hii ya habari?
Ni kiashiria cha ujinga tu wa watanzania hakuna zaidi.
 
Mbona ni kawaida kwa chombo cha habari kuchapisha habari mtandaoni na kuindoa. Hakuna tatizo wala kiashiria chochote hapo.
 
Wakuu habari,
Katika hali ya kushangaza azam tv kwenye kurasa zake za mitandao mbalimbali waliweka video zikimuonyesha Lissu akichukua fomu za kuwania urais kweny ofis za Nec huko Dodoma lakini muda mchache wakazifuta hizo post zote,hii inaashiria nini kwenye tasnia hii ya habari?
Ni kiashiria cha ujinga tu wa watanzania hakuna zaidi.
 
Wakuu habari,
Katika hali ya kushangaza azam tv kwenye kurasa zake za mitandao mbalimbali waliweka video zikimuonyesha Lissu akichukua fomu za kuwania urais kweny ofis za Nec huko Dodoma lakini muda mchache wakazifuta hizo post zote,hii inaashiria nini kwenye tasnia hii ya habari?
Ni kiashiria cha ujinga tu wa watanzania hakuna zaidi.
 
Wakuu habari,
Katika hali ya kushangaza azam tv kwenye kurasa zake za mitandao mbalimbali waliweka video zikimuonyesha Lissu akichukua fomu za kuwania urais kweny ofis za Nec huko Dodoma lakini muda mchache wakazifuta hizo post zote,hii inaashiria nini kwenye tasnia hii ya habari?
Shauri yao,la maana kwetu mgombea wetu amechukua form bila mizengwe. Tunajua kuwa media houses zote zimepokea maagizo toka kuzimu. Tutawafikia wapiga kura ana ana kwa na watatuelewa.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom