Azam TV uhuni mnaoufanya ulishafanyika miaka mingi. Serikali angalieni hili

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,321
11,410
Kujifanya mmepunguza bei ya vifurushi wakati in real sense mmehamisha zile channels ambazo angalau zinaonekana kupendwa ni uhuni ambao hatutegemei TV kama Azam ya Watu wa Dini watufanyie.

Ni kinyume na Imani yetu kabisa. Binafsi nanunua Azam kwa sababu ya VPL tu sababu home nmejaribu sana washawishi lakini wamegoma wakionekana kuipenda kufa DSTV.

NACHOOMBA KWA SERIKALI/WIZARA YA HABARI KWA KUSHIRIKIANA NA TFF.

Haki ya kuonesha Ligi ya Vodacom wapewe na wengine. Ziwepo hata Kampuni mbili ili zenyewe zishindane kutupatia bei yenye ahueni.kama wakiendelea kuwa Azam peke yao kuna hatari ya kutaka kutunyanyasa sana wakijua hakuna la kuwafnya. Zikiwepo Kampuni mbili au tatu bei itakuwa ya kuwajali watanzania hawa maskini.

Tumeona unyanyasaji mkubwa kwenye makampuni ya simu, banks n.k sasa huku nako mnataka kutukamua halafu kisanii mnasema mmepunguza bei? Astaghafilullah. Kwanini mwatutendea hivi?

IMG-20201125-WA0028.jpg
 
Wamefanya kazi kubwa Sana kwenye kampeni za mwaka huu kuliko media yoyote hapa bongo sahau kuona Serkali kuliingilia Kati....
 
Mi mwenyewe nilijiuliza sana hili swali, yaani TV ya kitanzania ipunguze bei kirahisi rahisi hv hv? Kimsingi hapo wamepandisha bei kihuni tu. Yaani kwa mimi niliyekuwa nanunua kifurushi cha elfu 18 ili niangalie mpira wa bongo ina maana sasa ili niangalie mpira natakiwa ninunue kifurushi cha elfu 20.

Tatizo mamlaka zetu zitakaa kimya tu kwa sababu ilo halina maslahi ya kisiasa.
 
Sijakilipia muda sana niliposikia hilo punguzo nikasema nilipie kumbe hakuna kitu, hao jamaa hawafai wamehamisha channels kihuni kweli bora zingebaki vilevile kuliko huo ujinga walioufanya
 
Wazinguaji na wamefanya uhuni tu, nalipia Azam kwa sababu ya ligi za kibongo tu sasa zamani Nilikua nalipa 18,000 sasahv itabidi nilipe 20,000
 
Wenye dstv tuwekeeni mchanganuo hapa tufanye maamuzi tuwaache wazee wa swala 5,nilishaachaga kulipia kitambo
 
Sasa elfu 20 nayo hela?.
Njoo DStv ujionee.
Mi mwenyewe nilijiuliza sana hili swali, yaani TV ya kitanzania ipunguze bei kirahisi rahisi hv hv? Kimsingi hapo wamepandisha bei kihuni tu. Yaani kwa mimi niliyekuwa nanunua kifurushi cha elfu 18 ili niangalie mpira wa bongo ina maana sasa ili niangalie mpira natakiwa ninunue kifurushi cha elfu 20.

Tatizo mamlaka zetu zitakaa kimya tu kwa sababu ilo halina maslahi ya kisiasa.
 
Watu mnalalamika sana...cement imepanda..sukari imepanda..gharama za maisha zimepanda pia...azam kupandisha hyo 2000 mnalalama kama nn..mbona mitandao ya simu inapandisha bei za vifurush mara kibao

Alafu muelewe kitu kimoja...azam wamebadili azam sport kutoka mwonekano wa kawaida kwenda HD..Sasa picha inaonekana vzr then unataka bei ibaki ileile kweli?then kwa sasa wanaonyesha karibu mech zote za ligi ya bongo,unadhan cost za kuonyesha live mechi zote hizo ni rahisi!?
 
Back
Top Bottom