Azam Tv: Naomba ufafanuzi wa malalamiko yangu kuhusu michezo

Ta Kamugisha

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,536
2,187
Kwanza nikupongeze kwa kuwa Sport Manager Azam Tv:
Nina malalamiko yafuatayo kuhusu Azam Tv hasa kwenye Sports:

1. Tunaomba uboreshe michezo kupitia Azam TV, TV yenu inatuonyesha Ligi Moja tu yenye maana duniani tofauti na mlivyokuwa mnajinasibu kuwa nyie ni TV ya michezo! Michezo ipi zaidi ya La liga na Ligi ya bara? Hapa badilikeni

2. Mmezidiwa na wachina au star times ambao wanaonyesha zaidi ya Ligi tano!

3. Arsenal TV, mlitutangazia kuwa mtatuwekea hii channel lakini mpaka Leo ni kimya! Hapa mmeniboa kinoma.

4. Inakuwaje kifurushi cha michezo kinachagua channel za michezo? Kwani ni fox sports, combat sports, MCs international sports hazipo kwenye kifurushi cha michezo?

5. Kwanini QTV inayorusha Ligi ya Ujerumani haifunguki?

6. Hili siyo la michezo: Hivi wale watangazaji wenu mliowachukua kwenye station tv zingine mbona hatuwaoni wakija na vipindi vya maana hapo Azam au mmewachukua ili iweje? Hama vipindi vya maana

Mimi kama mteja wenu naomba ufafanuzi kwenu Juu ya malalamiko yangu, la sivyo star times itawaangusha azam tv
 
Tatizo kubwa tv station zetu kila kitu ni kuigana na kufanya vitu kimazoea, binafsi siamini kama lundo la wanahabari waliochukuliwa toka vituo vngne wanaweza leta kitu kipya pale
 
Mh! Hili swala la kuchukua watangazaji kutoka TV mbalimbali ni zuri lakini lina risk unaweza ukajikuta umechukua makapi yaliyochoka ambayo hayana ubunifu tena wakati kuna vijana wapo vizuri wamesomea journalism wanasota mtaani
 
Ni kweli azam tv haijaweza kukidhi matarajio ya wateja wake.Wengi tulitegemea baada ya recruitment basi kinachofuata ni vipindi vya nguvu...

Kinachoshuhudiwa ni sura mpya kila siku huku vipindi vyenye mvuto vikiwa vichache sana.Ni azam news,mechi za la liga,mechi za vodacom na na vile vya msimu wa matukio ya live coverage kama live press,interview.....basi.Kile cha asubuhi wala sio kizuri kwakuwa kimekosa waongozaji wenye weledi wa kutosha.
Interview zao ni very predictable and limited to their poor knowledge on social issues.Kwahiyo kinaboa.

Nilitegemea kutakuwa na vipindi vizuri vya kisiasa baada ya kuwa na watangazaji wazuri wa mambo hayo kama Baruan Muhuza,Nurdin Selemani,Kaijage.Charles.Mhando etc lakini hamna kitu.Wote wamelundikwa kwenye taarifa za habari ambapo humo ni kama mnataka kumaliza kila kitu kwa hilo lisaa limoja.Hamtoweza.

Kwenye sports ndo balaa lingine.Baada ya kuanzisha chaneli ya azam sports nilitegemea zaidi ya mechi za laliga.Yaani hakuna hata pre and post match analysis sasa hivi.Mtu unashtukia tu mechi imeanza.Wako wapi wachambuzi mliotwambia siku mnazindua hii chaneli?Naona wachambuzi kwenye ligi yetu tu huku azam two.

Pia hiyo azam sports kwa nini msiifanye kama chaneli za supersports.Yani kuwe na vipindi vya kuongelea sports hasa football kila siku sio siku ya mechi tu.Jamani mbuni basi hata kipindi cha kuangazia mechi zolizofanyika sehemu mbalimbali duniani.Hata basi kuchambua magoli yaliyofungwa au ubora wa mchezaji mmojammoja kwenye mechi husika n.k.Charles Hilary wewe ni mtu wa mpira na hapa unaelewa kabisa ninachozungumzia.
Kwenye ligi ya vodacom mnaweza kuwa na kipindi cha goli bora labda la wiki au mwezi n.k
Kipindi cha baada ya taarifa ya habari i.e kipindi cha michezo kina muda mfupi sana.Bora hata kingekuwa kinaendelea azam sports kama huku two mnaendelea na hotuba au tamthilia!

Yaani azam sports imebakiza ligi ya la liga tu.Mngeiongezea thamani kwa kubuni vipindi vingine na kuongelea matukio kwenye ligi zingine kama epl mngeweza kuwashawishi hata wasio wapenzi wa hiyo la liga nikiwemo mimi kulipia hiko kifurushi chenu cha azam sports HD..Sasa ni la liga tu....na yenyewe pia ni mechi tu hakuna cha ziada.Badilikeni kwakweli.......
 
Kiukweli wanatukwaza hakuna jipya linaloonekana, wana vichwa vya maana lakini hakuna wanachofanya!

Mmeshindwa hata kutengeneza kipindi cha kuonyesha magoli ya Ligi ya Vodacom kila wiki! Wachambuzi mliokuwa nao wamewakimbia au hamuwalipi?

Tuwekeeni hata kipindi cha magoli ya EPL basi kama mmeshindwa hata kuonyesha mechi zao.

Mnazidiwa hata clouds kuchambua michezo na kipindi chao cha sport bar!

Hacheni uboya Azam TV, tunajivunia kuwa nanyi ila mnatuangusha,

Machanel ya kihindi cc wabongo yanatusaidia nn, mnashindwa hata kuwa na kipindi cha ngoma zetu au kuwa na kipindi cha kuelezea makabila ya Tanzania! Hata cha wanyama wa mbuga zetu Hanna!

Kweli ndio ubunifu wenu umeishia hapo? Ebu badilikeni basi
 
Kweli.....azam hawajafanya like tulichokitegemea. Wapo Na watangazaji mahiri lakini mpaka sasa hawajajionesha ubora wao.
 
Kweli mkuu hasa upande wa malipo kulipia Azam Sports sh.15,000 ili uone la liga na ligi kuu tu (only one channel) duh
 
Back
Top Bottom