Azam Tv na janja mpya

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,958
7,512
Hawa jamaa ni shida sana inabidi watiwe adabu. Wakiona unatumia king'amuzi chao pasipo kulipia vifurushi vyao ndani ya wiki mbili wanazima sehemu ya signal ili uwapelekee wajifanye wanakutengenezea bure lakini kumbe wanajifanya wanagusa gusa alafu wakishafanya yao wanakulazimisha lazima ununue kifurushi. Hili halina mjadala kwao.

Hawataki kabisa kuonesha zile chanel muhimu za ndani pasipo kulipia, hii janja yao iko technical sana na wanatumia mbinu hii kunyima wateja wao haki za free channels

Tunaomba TCRA waingilie kati na waichulie hatua Azam Tv
 
acha kupenda vya bure. kama una uwezo mdogo kama mimi weka hiyo kitu stoo kama mimi
mpaka ting wananipigiaga simu kuulizia kidude chao. mi sijui hata vilipo. ni utumwa kwa vihela vyetu hivi vya ngama kuanza kulipia hivyo vidude
tupa store
 
Guys kama kuna mtu anahitaji king'amuzi complete/full kit cha AZAM cha DISH ambacho ni kipya kabisa hakijamaliza hata mwezi na kimeshalipiwa chaneli zote kwa miezi mitatu. naomba anicheki DM tufanye biashara, kinapatikana kwa 165k (non-negotiable price)
 
Au kama kuna mtu ana king'amuzi cha DISH cha STARTIMES aje tubadilishane nimpe cha DISH cha AZAM but ataniongeza 60k ( NOTE: kingamuzi changu cha AZAM bado kipya hakijamaliza hata mwezi toka kinunuliwe na tayari kimeshalipiwa kwa muda wa miezi mitatu kwa chaneli zote )
 
Back
Top Bottom