Azam TV na Chanel ten wanaonyesha bunge hotuba ya wizara ya kilimo huku TBC wakionyesha vikatuni vya aeiou

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Wakati tukijua kilimo ni UTI wa mgongo wa uchumi wa taifa letu, leo muda huu waziri wa kilimo anawasilisha hotuba ya wizara hiyo.

Televisheni za Azam TV na Chanel Ten zinaonyesha live hotuba hiyo muhimu.

Cha ajabu, Televisheni ya taifa TBC muda huu inaonyesha vikatuni vya alfabeti vya a. e. i. o. u

Tafakari.
 
Kwani lazima chaneli zote kuonyesha bunge?

Kama wameshawasiliana na kuweka balance hiyo tatizo li wapi?

Vyombo vya habari karne hii vipo vingi so hawa wakionyesha hiki hawa wanaweza onyesha kile.. uzuri taarifa inaifikia jamii TBC hawawezi kuwa watimilifu kila siku.
 
Wakati tukijua kilimo Ni UTI wa mgongo wa uchumi wa taifa letu leo muda huu waziri wa kilimo anawasilisha hotuba ya wizara hiyo.

Televisheni za Azam tv na Chanel ten zinaonyesha live hotuba hiyo muhimu.

Cha ajabu

Televisheni ya taifa TBC muda huu inaonyesha vikatuni vya alfabeti vya

a. e. i. o. u

Tafakari.
Niliwahi kuuliza hivi TBC wanajitambua?????. Hawajui kama chombo hiki kinatakiwa kiwe cha Taifa na kwa maana hiyo kijikite kwenye majukumu ya kitaifa!!!!!. Sasa naona kila siku kiko kwenye kampeni za kisiasa. Kuna mtangazaji mmoja huwa anaongea kusifia hadi mishipa inamsimama aakimsifia kiongozi mmoja kuwa ni mzalendo namba moja. Binafsi huyu mtangazaji nikimuona tu na TBC yenyewe nafunga. Nafikiri anafagilia Ukuu wa wilaya. Wengi wameshamsoma Mh. ukimsifia tu anakuteua
 
Kiherehere chako na kisebusebu kinuka kwapa kilichokupeleka kushika rimoti ya shemeji yako kutafuta TBC wanaonesha nini usituletee hapa,,
 
Back
Top Bottom