nasaluka
Senior Member
- Jun 20, 2015
- 149
- 184
Hivi huyu pascal anahadhi ya kuitwa mwandishi kweli! Maana inaonekana huwa anahoja nyepesi na zenye lengo La ubishi na kubuy time tuPaskali,
Unasema wewe umekuta neno tukufu linatumiwa kueleza mapinduzi
kwa hiyo hukuona sababu ya kutaka kujua kwa nini mapinduzi yaitwe
''matukufu.''
Hivi wewe kama mwandishi hutaki ''to go an extra mile,'' katika uandishi
wako ukataja kujua zaidi?
Nimeeleza kuwa mapinduzi hayawezi kuwa na utukufu je unakubaliana
na sababu nilizoweka?
Unajaribu na kujitahidi kukwepa lakini ukweli ni kuwa unayapamba mauaji
kwa chuki uliyokuwanayo.
Post zako zote hapa ni shahidi.
Unasema wewe hukuwepo wala mimi sikuwapo.
Umekosea.
Mimi nilikuwapo na baba yangu alikuwa na uhusiano mkubwa sana na
jamaa wengi kutoka Zanzibar toka miaka ya 1950s au kabla.
Kwenye varanda ya nyumbani kwetu ukutani kulikuwa na picha moja
waki vijana watatu.
Katikati alikuwa baba yangu, Salum Abdallah na pembeni alikuwa Jaha
Ubwa na Abdulaziz Twala.
Picha hii ilipigwa kabla ya mapinduzi.
Baada ya mapinduzi Jaha na Twala waliuliwa na baba yangu hakuweza
kuitazama hii picha akaitungua ukutani na sijui iko wapi.
Nina kumbukumbu ya ''June Riots,'' za 1963 kwa kuona katika gazeti la
Ngurumo nyumbani ingawa sikuwa nafahamu kwa uhakika nini khasa
kilikuwa kinaendelea huko Unguja na wazee wakizungumza nami nikisikia
mazungumzo yao.
Watu wa Dar es Salaam walikuwa na uhusiano wa karibu sana na watu wa
Zanzibar kwa hiyo vurugu zilizokuwa zinatokea visiwani zikiwagusa sana.
Mapinduzi yametokea wazee walikuwa na shauku ya kutaka kujua hali ya
jamaa zao kama wako salama au vipi.
Hii ndiyo yangu mimi kuwa ingawa sikuwa Zanzibar lakini nilikuwa najua kuwa
yametokea mapinduzi visiwani.
Katika jamaa zetu waliouawa nimekutajia Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala
lakini mauaji na mateso kwa baadhi ya jamaa zetu hayakuisha hapo na nilikuwa
wakati mwingine nikimsikia mzee akizungumza kwa sauti zay chini akiulizia mtu
fulani na fulani na inapokuwa habari hazikuwa nzuri akiinamsiha kichwa chini.
Wakati ule nilikuwa na umri wa miaka 14.
Nadhani unaweza kuona kwa haya machache ni kiasi gani wengi wetu tumeathirika
na tunasikitika sana tunapokusoma.
Au ndo uandishi wa mtandaoni(kila MTU mwandishi)!?
Embu leta kazi zako zinazotokana na primary source km mzee Mohammed anavyofanya