Azam TV Limited yaingia mkataba wa kuonesha Matangazo ya Ligi Kuu kwa miaka 10. Mshindi misimu mitatu ijayo kulamba bonus Tsh 500m

Headcorner

Senior Member
Nov 26, 2020
188
277
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi na Azam TV Limited kwa pamoja wameingia makubaliano ya kuonesha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa muda wa miaka 10 wenye thamani ya Shilingi bilioni 225.6.

Kiasi hicho ni kikubwa zaidi kuwahi kutokea Afrika Mashariki na kuifanya thamani ya soka ya Tanzania kuongezeka.

BINGWA WA VPL kwa misimu mitatu ijayo, atapata TSH MIL 500 kama 'Bonus' kutoka Azam TV

Pia
Mshindi 2: Tsh Mil 250
Mshindi 3: Tsh Mil 225
Mshindi 4: Tsh Mil 200


AZAM.jpg
 
Tunaweza kusema ni ndogo ila mkataba kabla ya huo ilikua 23Bln kwa 5 years so hela ya miaka 5 inapatikana kwa mwaka mmoja sio mbaya kwa kuanzia kadri ya muda thamani inapanda

NB. Bingwa wa Vpl atapata 500Mln kama bonus kutoka kwa mdhamini so next contract ya Vodacom inabidi wajipange
 
Kaka hata kwa hesabu ndogo kiasi gani hio sio pesa ndogo imagine simba ndio club yenye mkataba mnono kwa sasa na ana mkataba wa billion 2.5 per year toka vunja bei sasa chukua bilion 225 gawanya kwa mwaka unapata bilion 22.5.

Zigawe kwa vilabu 16 vitavyocheza ligi kuu msimu ujao unapata karibia billion 1.5 kwa club sasa unakuaje mkataba mdogo tena wenye kuwa na muda wa miaka 10 na ukizingatia ligi yetu kiuhalisia ni chenga na utopolo mtupu.

Tuwape hongera Azam kwa kutufikisha Hapa mwaka 2011 kurudi ulikuwa huwezi hata kuona mechi yoyote bongo labda Simba na Yanga tena kwa low quality na nina uhakika tulikua hatuoni madudu ya marefa na ubovu wa team za ligi ilikuwa ni ukanjanja mtupu kabla.

Azam media group wamefanya makubwa hata kuwa na team nzuri hata huo ubora simba na yanga wanajisifu nao Azam wamechangia pakubwa mno.

Kwa wale wanaoona ni pesa ndogo watuoshe macho kimahesabu
 
Back
Top Bottom