Digaller
JF-Expert Member
- Oct 20, 2009
- 745
- 427
Nadhani tatizo ni operating system ambayo inatumiwa na azamtv haipo unfit kwa kuweka vikorombwezo vingi.Hili tatizo lingeisha kwa kuweka program ya mteja kutafuta ratiba mwenyewe. DSTV ukiweka channel 220 ukabonyeza OK inakupa option ya kutafuta unachokitaka kitaoneshwa wapi na muda gani?
Kwa AZAM TV sijaona program hiyo labda kama ipo anayejua anijulishe. Wakiweza kuweka hilo itakuwa rahisi sana, unachukua remote asubuhi unasearch ratiba unakuwa unajua mechi fulani itakuwa saa ngapi muda Fulani maana DSTV wameweka mpaka option ya "Reminder", ukitaka kuangangalia kipindi Fulani cha muda wa baadaye unabonyeza reminder muda ukifika decorder inaswitch yenyewe kwenye channel yenye kipindi unachotaka.
Ile os wanatumia dstv nadhani ni ubuntu au linux ipo vizuri sana, unaweza ibebesha mzigo mkubwa na ikawa imara.
Azamtv nadhani waachane na wachina na hizo booting system zao ambazo ndani ya dakika 1 inakuwa tayari iko loaded.