Azam TV Imefeli kwenye kujitangaza, haijulikani mechi inazoonyesha hadi ubahatishe, walio kitengo cha Promotion wang'olewe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,600
218,001
Hili ni tatizo la muda mrefu la Azam TV, hawana mabingwa wa promotion , huwezi kujua mechi inayochezwa hadi uingie kwenye channel ya soka , kwa mfano hakuna matangazo yoyote kwenye channel zao yanayoonyesha kwamba kuna ligi ya ufaransa , wala haijulikani game gani inaonyeshwa na channel fulani.

Wako duni mno kwenye eneo hili na wanaachwa nyuma kabisa na DSTV ambao hata channel ya sinema inakueleza gemu gani iko channel gani tarehe ngapi , yaani hawa Azam wanataka tuotee tu , wale wanaoangalia sinema zetu wala hakuna tangazo lolote linaloonyesha kama channel fulani inaonyesha game fulani ! wala hata mkanda unaotembea kama wafanyavyo super sports , haya ni maajabu ! na ni aibu kwa wahusika.

Biashara yoyote ni matangazo , Kwani kuna ugumu gani kutembeza hata mkanda wa maandishi kwenye kila channel yenu kuonyesha mechi fulani itachezwa tarehe fulani na itaonyeshwa kwenye channel fulani?

Kwa mfano, unaweka mechi kisirisiri kwenye ZBC2 huku ukijua hiyo ni channel ya misikiti unadhani ni nani atajua kuna gemu huko ? Kama lengo lenu ni kutufanya tuangalie hizo mechi basi ni lazima mtutangazie Mechi gani iko channel gani na ni saa ngapi , iwe EPL , BUNDESLIGA, CARABAO, NBC, YA KIRAFIKI AU YOYOTE.

Acheni kuzifanya mechi za soka kuwa siri yenu.
 
Aseee mbona mi nimeona tangazo UTV na kifurushi hata sijalipia aseeee
 
Azam wana utaratibu mbovu sana wa kuonyesha mechi ,channel za mpira Azam hazifiki 4 lakini anataka aonyeshe ligi 1 bundasliga ,ligi kuu,Mara mechi hii iko kwenye extra ,nyingine ipo ZBC2 wanashindwa hata na Chanel ya 24hrs ya Kenya wanakujulisha mechi za weekend za EPL,liga 1 ,bundasliga watakazorusha
 
Azam wana utaratibu mbovu sana wa kuonyesha mechi ,channel za mpira Azam hazifiki 4 lakini anataka aonyeshe ligi 1 bundasliga ,ligi kuu,Mara mechi hii iko kwenye extra ,nyingine ipo ZBC2 wanashindwa hata na Chanel ya 24hrs ya Kenya wanakujulisha mechi za weekend za EPL,liga 1 ,bundasliga watakazorusha
Bila matangazo ni sawa na kuibia wateja wao
 
Ukitoa ajira kwa kufuata mlengo fulani tena wa kibaguzi unategemea upate maendeleo na ubinifu....?!

Ubaguzi wowote huwa unazaa umauti .....
Aiseee, UDINI utatuua, mungu atusaidie hii chuki ya dini ibaki level hii hii, ukivuka kidogo hapa, tutapata vita vya wenyewe kwa wenyewe, ama mabo ya kimbari..

Alimuajiri bosi mkuu bwana tido muhando, bosi mkuu wa michezo pale bwana PATRICK kahemele, nani sijui jina limenitoka, na wafanyakazi kibao wasio na dini yake.

Mzee toa kichwani hayo mawazo mgando, mtazalisha chuki kubwa kwa vizazi vyetu vijavyo.
 
Aiseee, UDINI utatuua, mungu atusaidie hii chuki ya dini ibaki level hii hii, ukivuka kidogo hapa, tutapata vita vya wenyewe kwa wenyewe, ama mabo ya kimbari....
Kuna Baraka Mpenja
Patrick Nyembera
Charles Hilary
Ivona Kamuntu

Mkuu , hawa jamaa wanasumu nyoyoni mwao za chuki dhidi ya SSB & Company.

Ila management haina shida kabisa ipo Well balanced na kuajiri quality people.
 
Back
Top Bottom