Azam Sports Federation Cup Live Uptades leo Tarehe 23-1-2016

mkolaj

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
3,020
1,087
Nawaarifu Wanamichezo wote leo tukutane hapa kupeana Updates zitakazokuwa zinajili viwanjan katika ule muendelezo wa kombe la FA.
Leo katika uwanja wa Jamhuri Morogoro timu ya Burkina Faso watawakaribisha Simba SC ya Dar es salaam.
Kule Mwanza Pamba watakuwa wenyeji wa Toto Africa. Michezo yote itaanza saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Kwa upande wangu naitakia kila la kheir timu ya Burkina Faso katika mchezo wa leo.
 
[QUOTE="sembo]

Huku akishuhudiwa na mashabiki lukuki waliofurika katika uwanja wa Jamuhuri, uliopo mjini Morogoro.. Yule Mnyama hatari mwituni, Simba S.C aunguruma tena.
Na hii ni baada ya kuwakung'uta bila huruma, goli 3-0 Bukina Faso.

Mechi hii ilikua ni ya kuwania Kombe la Shirikisho.. Walioacha kilio kikubwa kilichojaa simanzi nyingi kwa mashabiki wa Bukina Faso na Ndala, katika mji kasoro bahari, Moro ni Hamis Kiiza [dk.78 na dk. 90] na Mwinyi Kazimoto a.k.a Ball Dancer [dk. 90].

Japo mashabiki wa Bukina Faso na Ndala wametoka wakiwa vichwa chini.. Ila wameshindwa kabisa kuficha chuki zao kwa Mnyama na kuanza kulisifia soka maridadi walilotandaza leo vijana wa Mayanja.. Kwa kifupi hapa mjini Moro... Leo ni Simba S.C kila kona.

Jackson Mayanja.
Katika mechi zake 3 alizoiongoza Simba S.C kama Kocha Mkuu.. Timu imeshinda mechi 3.. Imefunga magoli 6.. Imefugwa magoli 0.

Naziona neema zinakuja.. Chini ya Mayanja
[/QUOTE]

Goooo
 
Safiiii.....mdogomdogo tunakamata mwizi kimyakimya....madogo walitulia tunalitwaa hilo na tunaenda CAF mwakani
 
Mm naomba kuelimishwa kuhusu hili kombe la FA maana nasikia tuu ligi inasimamishwa kwa ajili ya kombe la FA ni club gani zitashiriki na mshindi atakuwa na title gani?.
 
Mm naomba kuelimishwa kuhusu hili kombe la FA maana nasikia tuu ligi inasimamishwa kwa ajili ya kombe la FA ni club gani zitashiriki na mshindi atakuwa na title gani?.
1)bingwa wa VODACOM bara anawakilisha klabu bingwa Afrika. Wapili VODACOM haendi kokote
2)bingwa wa hii FA anawakilisha kombe la shirikisho Afrika

Timu za ligi daraja la kwanza na level za chini zilianza kupunguzana raundi za awali kisha waliopona ndio wakajumuishwa na za ligi kuu kuendelea na hiyo ligi ambayo ndio inaanza msimu wa 2015/2016. Mdhamini ni Azam
 
Zilianza timu za ligi daraja la pili na madaraja ya chini raundi ya kwanza, zilizobakia zikapambanishwa na za daraja la kwanza raundi ya pili, baada ya hapo zilizobakia zote zinapambanishwa na za premier league raundi ya tatu itaendelea hivyo mpaka apatikane bingwa atakayewakilisha nchi kwenye kombe la SHIRIKISHO.
 
Japo kipindi cha kwanza tulibanwa sana.Nashukuru tuna vijana bora kama Ndemla wamefanya mambo.
 
Sasa kwa mfano Simba akashinda hili kombe na akawa mshindi pia wa ligi kuu(as it is going to be) itakuwaje? Au atacheza club bingwa na kombe la shirikisho mwenyewe?
 
Back
Top Bottom