Azam Sinema Zetu punguzeni kukatakata tamthilia

Kitorondo

Member
Oct 21, 2011
61
33
Azam Sinema zetu mmeleta ubunifu mzuri wa kuwapromoti wasanii wa filamu na wengi wanacheza filamu nzuri, tatizo linakuja kwa Wahariri kukata baadhi ya tamthilia na kuweka matangazo ambayo mengine wala siyo ya biashara ambayo hayakupaswa kuingizwa katikati ya tamthilia.

Tamthilia ambazo zinaongoza kwa kukatwa ni Panguso ambayo inapaswa kuonyeshwa dakika 30 lakini ukichunguza utagundua ni dakika 10 au 15 tu na dakika zingine zimekatwa kwa kucheleweshwa kuanza kipindi kwa dakika nyingi na kuweka matangazo mara kwa mara ambayo wala si ya kibiashara mfano kuweka tangazo la tamthilia nyingine katikati ya Panguso.

Utakuta vinaonyeshwa vipande vinne tu tamthila inakwisha hadi kesho.

Kwa Waigizaji wa Panguso ningependa kuwashauri kupunguza muda wa matukio mfano wa kulia unakumta mtu anachukua muda mrefu kulia badala ya kupeleka kwenye tukio lingine hii nayo inawachosha watazamaji.

Kuna kosa la kiufundi kwenye vyeo vya Inspekta Kilonzo na Inspekta Lwambano. Kimsingi Mkuu wa Upelelezi wa Jinai nchi nzima hawezi kuwa na cheo cha inspekta wangeweza kumwita Inspekta Lwambano Kamishna msaidizi au Naibu DCI na Inspekta Kilonzo Kamishina au DCI, lakini wote wana vyeo sawa vya Inspekta lakini Kolonzo ni bosi hawezi kuwa inspekta angalau wangeanzia kwenye vyeo vya Mrakibu au mrakibu mwandamizi hadi Kamishna.

Tamthilia nyingine ni Shilingi.

Muda wake unasomeka dakika 60 liakini hapa katikati inakatishwa sana kwa mambo yasiyokuwa ya lazima na kuwakera watazamaji.

Mambo haya Azam mkiyarekebisha mtakuwa namba 1.

Ushauri wangu ni huo.
 
kumbe we nae umeona hilo na kwenye tamthilia za Azam two hua ni dakika 60 lakin matangazo sasa ni mengi afu sio ya biashara ni yao yao ya ovyo tu tamthilia inachukua dakika 20 kuisha
 
Back
Top Bottom