Azam Marine Wanatumaliza Na Nauli Holela

Majembe

Member
Jun 18, 2008
35
5
Habari ya wiki endi ndefu wa ndugu wa familia ya Jamii forum, nina imani wote mpo salama.

Napenda kuwakilisha hii habari ili mlifahamu ili na kulichambua kwa umoja wetu.
Usafili wa Boat ni muhimu hasa kwa wenzetu wa Unguja, pemba na sehemu nyingine zote zinazofikikika kirahisi na usafiri wa aina hii, kinachosikitisha ni kua wamiliki wa vyombo hivi hawana lengo la luisaidia jamii badala yake ni kuwaumiza, nina imani wote tunafahamu kuhusiana na kupanda kwa bei ya petrol lakini sioni sababu ya hawa wamiliki kupandisha bei shilingi elfu 3000 kwa mara moja ina maana kila abiria analazimika kuinunulia boat anayopanda lita mona na nusu ya petrol!!! hii imenishangaza na bado kwenye matangazo yao ndani ya boat hizo mnatangaziwa kuwa nauli ni 18,000 wakati umeinunua ticket ulipondia humo boatini kwa 22,000 mimi naona huu ni unyonywaji wawanyonge hivi hawa SUMATRA wanalifahamu hili na lini walitangaza kua bei mpya za usafiri wa boat Dar-ZNZ ni 22,000? naomba hili nalo tulifanyie kazi ndugu zangu mwisho hata kwenda kwenye misiba tutashindwa kwa mtindo wa kuamka na kukuta bei imebadirika.
 
FairPlayer

JF-Expert Member
Feb 27, 2006
4,144
703
Panda Ndege kama boat ni ghali. Au panda Mtumbwi au mashua bei zao zipo chini sana!

Punguza kulalamika, do something!
 
wewe hili jina halikufai wewe si fairplay kama unavyojiita nakuomba ubadiri jina, tunapolalamokia mafisadi na huu pia ni ufisadi na simaanishi kua mimi nashindwa kulipa hiyo nauli tuelewe kua Tanzania inaidadi kubwa ya walala hoi iyo usipinge na kama wewe nimmoja wa mafisadi wasiojali wenzao iweke wazi ieleweke, kila siku wavuvi wasio na idadi wanakufa na mitumbwi halafu unadai abiria wananchi wapande mitumbwi kweli wa Tanzania hatupendani lazima ni ndugu wa Rostam,Chenge na Lowasa wewe!!!!!!
 
NaimaOmari

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
801
45
Habari ya wiki endi ndefu wa ndugu wa familia ya Jamii forum, nina imani wote mpo salama.

Napenda kuwakilisha hii habari ili mlifahamu ili na kulichambua kwa umoja wetu.
Usafili wa Boat ni muhimu hasa kwa wenzetu wa Unguja, pemba na sehemu nyingine zote zinazofikikika kirahisi na usafiri wa aina hii, kinachosikitisha ni kua wamiliki wa vyombo hivi hawana lengo la luisaidia jamii badala yake ni kuwaumiza, nina imani wote tunafahamu kuhusiana na kupanda kwa bei ya petrol lakini sioni sababu ya hawa wamiliki kupandisha bei shilingi elfu 3000 kwa mara moja ina maana kila abiria analazimika kuinunulia boat anayopanda lita mona na nusu ya petrol!!! hii imenishangaza na bado kwenye matangazo yao ndani ya boat hizo mnatangaziwa kuwa nauli ni 18,000 wakati umeinunua ticket ulipondia humo boatini kwa 22,000 mimi naona huu ni unyonywaji wawanyonge hivi hawa SUMATRA wanalifahamu hili na lini walitangaza kua bei mpya za usafiri wa boat Dar-ZNZ ni 22,000? naomba hili nalo tulifanyie kazi ndugu zangu mwisho hata kwenda kwenye misiba tutashindwa kwa mtindo wa kuamka na kukuta bei imebadirika.

Majembe ... ukichelewa tu kununua ticket unalanguliwa mpaka elfu 30,000.. halafu ukiwa na mzigo tu kidogo wanakuchaji .. au kuna siku walizuia kabisa watu kupita na vifuko size ya rambo ile ya Shs. 150 imagine .. wakawaambia wasubiri flying horse . Vyakula ghali ... kule mtu anashindwa hata kubeba chochote ... wanatuua kweli yafaa wa control bei zao
 
FairPlayer

JF-Expert Member
Feb 27, 2006
4,144
703
wewe hili jina halikufai wewe si fairplay kama unavyojiita nakuomba ubadiri jina, tunapolalamokia mafisadi na huu pia ni ufisadi na simaanishi kua mimi nashindwa kulipa hiyo nauli tuelewe kua Tanzania inaidadi kubwa ya walala hoi iyo usipinge na kama wewe nimmoja wa mafisadi wasiojali wenzao iweke wazi ieleweke, kila siku wavuvi wasio na idadi wanakufa na mitumbwi halafu unadai abiria wananchi wapande mitumbwi kweli wa Tanzania hatupendani lazima ni ndugu wa Rostam,Chenge na Lowasa wewe!!!!!!

Lete solution acha kulalama. Mafuta yamepanda bei kila mtu anajua. Kama unalanguliwa toa taarifa polisi au kwa PCCB. Ina maana hujui kulanguliwa ni kosa?

Halafu think positively, toka lini Rostum akawa ndugu wa Lowassa na Chenge? hao watu hawahusiani.

Njoo na solution ya tatizo lako tumechoka kusikia lawama!

Fairplayer
 
nimewafanisha wewe, Lowasa, Chenge na Rostam kwakua wote ni ndugu wa familia moja inayokua kwa kasi ya FISADI family na si kwarandi wala kabira.

kama hukukurupuka kusoma ungeona nimesema bei imepanda kila mtu anajua lakini kuileta humu ni ili kila mtu ajue na kuchangia kwa anachokijua juu ya hili kama Sumtra wapo na kudhibiti bei ni kazi yao ndio maana nimeileta hapa kwa imani kua watu wengi wanasoma hivyo itawafikia walengwa. ningekuwa na imani na PCCB na Sumatra nisingeleta hii mada hapa.
 
Majembe

Member
Jun 18, 2008
35
5
Majembe ... ukichelewa tu kununua ticket unalanguliwa mpaka elfu 30,000.. halafu ukiwa na mzigo tu kidogo wanakuchaji .. au kuna siku walizuia kabisa watu kupita na vifuko size ya rambo ile ya Shs. 150 imagine .. wakawaambia wasubiri flying horse . Vyakula ghali ... kule mtu anashindwa hata kubeba chochote ... wanatuua kweli yafaa wa control bei zao

mfano Ijumaa iliopita na jumamosi ndio hasa bei ilikua ya ajabu kisa abiria wengi kwakua wanaenda 77 kiukweli hakuna chombo cha kusimamia hizi bei za usafiri wa aina hii kila boat ina bei yake zenye bei ya chini abiria wanajazwa mpaka wanasimama bado na AC hazifanyi kazi si kuuana huku.

Ninachoongelea hapa kongeza elfu 3000 kwa mara moja ni nyingi sana kwa mTZ wa hali ya chini na haimaanishi masikini afe kwakua hana hela yake inatosha kupanda mtumbwi. Serilaki iliangalie hili na itaafute ufumbuzi yote kwakua hivi vyombo ni vya watu binafsi wanaojali maslahi yao bila kujali hali halisi ya maisha.
 
Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,955
4,388
Mtoto wa fisadi utamjua tu.
Yeye hafikirii kuna watu wanaishi kwa jelo kwa siku wengine ndo hivyo tena.
Kuna watu wanapoteza maisha kwa kukosa buku ya matibabu kila siku tunasikia.
Fisadi akiumwa tu India kupata matibabu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom