Mavipunda
JF-Expert Member
- Jun 27, 2012
- 7,005
- 7,734
Katika hali ya kushangaza wala kutoa taarifa kwa Umma kampuni hii inayomilikiwa na Bakharesa imepandisha nauli kwa baadhi ya madaraja katika boti zake zinazosafiri katika ukanda wa Bahari ya Hindi. Kwa sasa Royal Class inakuwa 60,000 badala ya 50,000 na VIP Class inakuwa 50,000 badala ya 40,000. Madaraja ya Bussiness na Economic yanabaki kama ilivyo sasa 35,000 na 25,000,ila kuna tetesa kwamba watapandisha
Cha kushangaza mabadiliko hayo yamefanyika jana tu bila ya umma kujuulishwa yaani taarifa unazipata counter ukienda kukata tiketi. Huu ni uhuni kwa kampuni kubwa kama hii inayomiliki vyombo vya habari. Na je SUMATRA wana taarifa na wamebariki mabadiliko hayo ya nauli?Kuna tetesi kwamba wanataka kufidia kodi wanayaodaiwa kutokana na KASHFA ya BANDARI KAVU kupitia migongo ya wavuja jasho.
Ila cha kushukuru Fast Jet wameanzisha safari za Dar to Zanzibar bila ya shaka bora ukalipe nauli ya 35,000 kwa kusafiri kwa muda mfupi robo saa kuliko kulipia hela hiyo hiyo na kuteseka na mawimbi na masimango ya wafanyakazi wa Bakhasa kwa masaa 2