Azam kufuta Post za CHADEMA: Ujumbe mzuri kwa Media za Tanzania

mzee wa liver

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
78,941
414,656
Na Malisa

Nimekuwa nikisoma kwenye vitabu na sasa nashuhudia kwa macho. Uhuru wa habari unakanyagwa na watu hawathubutu kukemea kwa sababu ya HOFU. Vyombo vya habari vilivyoalikwa kuripoti tukio la Lissu kuchukua fomu havijatokea kwa sababu ya HOFU

Azam wakavuka kiunzi cha HOFU na kwenda kuripoti. Lakini ghafla wakakatisha matangazo na kufuta post zote zinazohusu Lissu kuchukua fomu. Nimeshangaa sana

Kuna watu wanashangilia kuona uhuru wa habari ukiminywa ili wafurahishe mamlaka. Na wengine wanaogopa kukemea ili nao wasiingie kwenye makucha ya mamlaka. Tukifika hapa hakuna aliye salama.

Jana @advocate_jebra alieleza kisa cha Simba na Kondoo. Simba alifungiwa kwenye kizimba kwa siku kadhaa. Akawa anatafuta msaada wa kufunguliwa kwa nje. Kondoo akapita. Simba akamwambia nifungulie naahidi sitakula. Kondoo akamwambia Simba apa, akaapa. Kondoo akamfungulia.

Alipotoka akamrarua kondoo na kutaka kumla maana alikua na njaa ya siku kadhaa alizofungiwa kwenye kizimba. Wanyama wengine wakapita wakakuta Simba na Kondoo wakizozana. Kondoo akajielezea, Simba nae akajielezea. Simba akakiri ni kweli aliahidi hatamla kondoo lakini ana njaa ya siku 3 afanyeje?

Wanyama wote kwa sababu ya HOFU wakaunga mkono maelezo ya Simba kuwa amle tu kondoo, maana alikua na njaa.

Kobe akasema hajaelewa mkasa huo vizuri. Akamuuliza Simba unasema ulifungiwa kwenye kizimba? Simba akajibu ndio. Akamuuliza kipi? Akamwambia kile pale? Akamuuliza mbona kidogo sana? Uliwezaje kukaa humo? Simba akasema nilikuwemo. Kobe akamwambia hebu ingia tuone kama kweli uliweza kuenea humo. Simba akaingia, kobe akafunga komeo kwa nje na kuondoka.

Kobe akawaambia wanyama wenzie. Leo Simba angemla kondoo mngejiona mko salama kwa sababu si nyie mmeliwa. Lakini kesho angepata njaa tena, na hatujui ingekua zamu ya nani.

Ukiogopa kukemea uonevu haimaanishi kwamba upo salama. Inamaanisha umejiweka kwenye hatari zaidi. Leo vyombo vyote vimeungana na mamlaka kuzuia habari za Lissu. Nilipoona Azam wamerusha matangazo nikasema angalau tumempata Kobe wa kuokoa wenzie. Mara ghafla kobe huyo nae akaungana na wenzie kumtetea Simba amle kondoo. Bila kujua kesho Simba atapata njaa tena na hawajui itakua zamu ya nani. #Subhanallah
 
Hata mimi nilishangaa sana kuwaona AZAM TV wakiwa wamejitoa muhanga kurusha tukio hilo.

Sikufatilia mpaka mwisho kutokana na kuwa bize na shughuli. Nashangaa unaposema kuwa, kumbe baadaye walikata matangazo na kuingia mitini tena?

Basi hicho ni kituko cha mwaka...m!!
 
Wanaomiliki magazeti, radio na runinga mmezidi kuogopa. Yaani wamekuwa kama baradhauli wakimuona basha wanavua chupi kabisa. To hell na mlaaniwe yaani unamuogopa binadamu mwenzako kiasi hicho. Kwenye kampoeni itakuwaje, hiyo inaonesha kuwa vyama vya upinzani vitakosa coverage kwenye media. Hongera sana jamii forum kuruhusu clip za vyama vya upinzani kurushwa humu.
 
wanaomiliki magazeti, radio na runinga mmezidi kuogopa. Yaani wamekuwa kama baradhauli wakimuona basha wanavua chupi kabisa. To hell na mlaaniwe yaani unamuogopa binadamu mwenzako kiasi hicho. Kwenye kampoeni itakuwaje, hiyo inaonesha kuwa vyama vya upinzani vitakosa coverage kwenye media. Hongera sana jamii forum kuruhusu clip za vyama vya upinzani kurushwa humu.
Media za tanzania zimetiwa jiti mbele na nyuma
 
91 Reactions
Reply
Back
Top Bottom