Azam kufuta Post za CHADEMA: Ujumbe mzuri kwa Media za Tanzania

Ni hawahawa watu wa media wanaofungiwa vyombo vyao au kupigwa faini na Lissu amekuwa mtetezi wao subirini siku nchi hii ikipata Uhuru mtatafuta pa kutokea mbwa nyie.
Ubaya haulipwi kwa ubaya bwashee ,tuwaache tu
 
Chadema mmeonewa katika hili sio sawa tunahitaji usawa kwenye ushindani wa kisiasa nchini ili taifa listawi
 
Acheni kulalamika mlishindwa hata kuanzisha online tv?Sasa hivi ingekuwa na followers kibao leo mngerusha wote tungeangalia hapo. Mnajua kila kitu why msitafute solution mapema ?miaka mitano sasa Chadema online tv ni kulipa leseni na mngeitumia kueneza habari. Acheni ubahiri utawacost sana kipindi hiki cha kampeni.
 
Chadema nunua camera za video zimejaa madukani nunua kifaa cha kurusha matangazo live, kama blackmagic, live U solo, vidiu livestream, teradek live, mevo, go pro, teradek livestream. Ili mrushe matangazo yenu kupitia mitandao yenu ya youtube. Halafu mshare link na muwaambie watu wa subscribe. Wafuasi washare link kila sehemu. Muda wa kampeni hakuna tv wala redio wala online tv itakayo onesha mambo ya upinzani hata moja. Yaani inatakiwa channel yenu iwe na subscriber kama milioni 5 hivi. Kulalamika hakutasaidia kitu chochote. Warushe clip kupitia account zao au watumie instalive popote walipo ili ujumbe ufike.


Kulalamika hakutasaidia kitu.
Sasa bwashe bibi yangu aliyeko kule rombo mambo yaku subscribe anawezaje wakat kuliyamka tu ni shida
 
Sasa bwashe bibi yangu aliyeko kule rombo mambo yaku subscribe anawezaje wakat kuliyamka tu ni shida
Mkuu video ataoneshwa na wewe mjukuu. Au hata wajukuu wengine wenye simu za kisasa watamuonesha na kumsimulia. Msimu huu kuna wapiga kura zaidi ya milioni ishirini na tano. Na zaidi ya nusu yao ni vijana na wengi ni watumiaji wa mitandao na wengi wameathirika na maisha magumu pamoja na ukosefu wa ajira (ikiwamo mimi). Sasa kama wapinzani wasipojielekeza katika mitandao pamoja na vyombo vya habari watashindwa kupata kura za vijana. Kura zinatafutwa kwa mbinu na sio kwa kulalamika na kutukana.

Niishie hapo
 
Na Malisa

Nimekuwa nikisoma kwenye vitabu na sasa nashuhudia kwa macho. Uhuru wa habari unakanyagwa na watu hawathubutu kukemea kwa sababu ya HOFU. Vyombo vya habari vilivyoalikwa kuripoti tukio la Lissu kuchukua fomu havijatokea kwa sababu ya HOFU.

Azam wakavuka kiunzi cha HOFU na kwenda kuripoti. Lakini ghafla wakakatisha matangazo na kufuta post zote zinazohusu Lissu kuchukua fomu. Nimeshangaa sana.

Kuna watu wanashangilia kuona uhuru wa habari ukiminywa ili wafurahishe mamlaka. Na wengine wanaogopa kukemea ili nao wasiingie kwenye makucha ya mamlaka. Tukifika hapa hakuna aliye salama.

Jana @advocate_jebra alieleza kisa cha Simba na Kondoo. Simba alifungiwa kwenye kizimba kwa siku kadhaa. Akawa anatafuta msaada wa kufunguliwa kwa nje. Kondoo akapita. Simba akamwambia nifungulie naahidi sitakula. Kondoo akamwambia Simba apa, akaapa. Kondoo akamfungulia.

Alipotoka akamrarua kondoo na kutaka kumla maana alikua na njaa ya siku kadhaa alizofungiwa kwenye kizimba. Wanyama wengine wakapita wakakuta Simba na Kondoo wakizozana. Kondoo akajielezea, Simba nae akajielezea. Simba akakiri ni kweli aliahidi hatamla kondoo lakini ana njaa ya siku 3 afanyeje?

Wanyama wote kwa sababu ya HOFU wakaunga mkono maelezo ya Simba kuwa amle tu kondoo, maana alikua na njaa.

Kobe akasema hajaelewa mkasa huo vizuri. Akamuuliza Simba unasema ulifungiwa kwenye kizimba? Simba akajibu ndio. Akamuuliza kipi? Akamwambia kile pale? Akamuuliza mbona kidogo sana? Uliwezaje kukaa humo? Simba akasema nilikuwemo. Kobe akamwambia hebu ingia tuone kama kweli uliweza kuenea humo. Simba akaingia, kobe akafunga komeo kwa nje na kuondoka.

Kobe akawaambia wanyama wenzie. Leo Simba angemla kondoo mngejiona mko salama kwa sababu si nyie mmeliwa. Lakini kesho angepata njaa tena, na hatujui ingekua zamu ya nani.

Ukiogopa kukemea uonevu haimaanishi kwamba upo salama. Inamaanisha umejiweka kwenye hatari zaidi. Leo vyombo vyote vimeungana na mamlaka kuzuia habari za Lissu. Nilipoona Azam wamerusha matangazo nikasema angalau tumempata Kobe wa kuokoa wenzie. Mara ghafla kobe huyo nae akaungana na wenzie kumtetea Simba amle kondoo. Bila kujua kesho Simba atapata njaa tena na hawajui itakua zamu ya nani. #Subhanallah
#CHADEMA anzisheni kampeni ya ku-unfollow #azam media zote na kususia vingamuzi vyao
 
Back
Top Bottom