Azam:- Hakuna mafanikio ya haraka kiasi hicho.

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Nimemsikia msemaji wa Azam kupitia RFA kuwa:-
1. Kocha waliyemuajiri ni kutokana na uongozi wa klabu na sio mashabiki, hilo ni sawa lakini hakuna timu isiyokuwa na masabiki hata vilabu vya Simba (mnyama) na Yanga (mwananchi) vilianza kama vikundi tu vya watu wachache na leo pana mashabiki lukuki si ndani ya nchi pekee hata nje ya nchi hii.
2. Mafanikio ya kocha huyu alipokuwa na FC Leopard ni tofauti kabisa na atakavo kuwa na Azam kwa sababu ya lugha. Lugha ni kitu muhimu mno katika maisha ya binadam hivo kwa kuwa huyu hajui Kiingereza wala Kiswahili pana tatizo hapo. FC Bayern Munich walipomuajiri Pep walihakikisha anaifahamu vema lugha ya Kijerumani kwanza na ndipo wakamkabidhi timu, kumbuka Pep ni Mhispania. Sasa huyu kocha hajafundishwa Kiswahili na kama ujuavyo sie lugha ya Kiingereza hatukijui sawasawa itakuwaje?
Sitegemei mabadiliko ya haraka hapo Azam kama ndoto za viongozi wake zinavowatuma.
 
Azam bado wanaendesha timu kiswahili kama Simba na Yanga ,Stewart Hall amesema uongozi ulikuwa hadi unampangia wachezaji wa kucheza
 
Nimemsikia msemaji wa Azam kupitia RFA kuwa:-
1. Kocha waliyemuajiri ni kutokana na uongozi wa klabu na sio mashabiki, hilo ni sawa lakini hakuna timu isiyokuwa na masabiki hata vilabu vya Simba (mnyama) na Yanga (mwananchi) vilianza kama vikundi tu vya watu wachache na leo pana mashabiki lukuki si ndani ya nchi pekee hata nje ya nchi hii.
2. Mafanikio ya kocha huyu alipokuwa na FC Leopard ni tofauti kabisa na atakavo kuwa na Azam kwa sababu ya lugha. Lugha ni kitu muhimu mno katika maisha ya binadam hivo kwa kuwa huyu hajui Kiingereza wala Kiswahili pana tatizo hapo. FC Bayern Munich walipomuajiri Pep walihakikisha anaifahamu vema lugha ya Kijerumani kwanza na ndipo wakamkabidhi timu, kumbuka Pep ni Mhispania. Sasa huyu kocha hajafundishwa Kiswahili na kama ujuavyo sie lugha ya Kiingereza hatukijui sawasawa itakuwaje?
Sitegemei mabadiliko ya haraka hapo Azam kama ndoto za viongozi wake zinavowatuma.

miafrika ndo zetu kujifanya tunajua kila kitu hasa kwenye mamb ya hela..
 
Mkuu soka ila lugha yake na kujua kiswahili suo issue kabisa. Waulize yanga kama brandts anafundisha kiswahili au stewart alikuwa anafundisha kiswahili au kim poulsen anafundisha kiswahili. Soka lina lugha yake mkuu usiwe na shaka
 
Unajuwaje iwapo hicho sio chanzo kimojawapo cha yeye Stewart kuachia ngazi baada ya kuona anashindwa kuelewana si tuna wachezaji bali hata viongozi? Unajuwaje iwapo ndani ya nafsi zao, Brandts na Stewart wanarodhika na jinsi mafundisho yao yanavyopokelewa na kufuatwa na wachezaji wao?
 
Mkuu fuatilia soka duniani kote utagundua kuwa lugha sio kikwazo hata kidogo. Bahati njema kocha mpya wa Azam leo amenukuliwa na Mwanaspoti gazeti anaulizwa kuhusu lugha ametoa jibu kama nililoeleza jana kuwa Soka lina lugha yake moja tu duniani kote na hata wakutane mreno na mwingereza, wataelewana tu inapofikia kuwa wanafundishana soka. Lugha haijawahi kuwa kikwazo mahala popote duniani katika kufundisha soka mkuu.
 
Kwa Tanzania sio hivyo mkuu. Mfano angalia maneno 'Kamati ya Ufundi' kwa lugha ya kisoka ulimwenguni ni 'Technical team' kwa Tanzania ni kamati ya uchawi ambayo kila timu Tanzania hii, pamoja na Azam, lazima iwe nayo. Au 'tackling', kisoka ni mchezaji kujaribu kumpokonya adui mpira, lakini kwa lugha ya kiufusadi wa soka la Tanzania ni kumrubuni mpinzani. Iweje lugha isiwe kikwazo?
 
Mkuu soka ila lugha yake na kujua kiswahili suo issue kabisa. Waulize yanga kama brandts anafundisha kiswahili au stewart alikuwa anafundisha kiswahili au kim poulsen anafundisha kiswahili. Soka lina lugha yake mkuu usiwe na shaka

Lugha sio tatizo kwenye kufundisha, lakini mpira wa sasa ni zaidi ya kufundishana uwanjani tu. Kuna mambo mengi ambayo mwalimu anapaswa kuyasimamia. Mfano inasemekana kuwa Arsene Wenger ni Kocha bora wa mpira kuliko Sir Alex, lakini Sir Alex anamshinda Wenger Man Management, kucontrol behaviour mbalimbali za wachezaji nje na ndani ya uwanja. Kama Azam wanataka kwenda extra mile zaidi ya Simba na Yanga wanapaswa wazingatie hili.
 
Agreed 100%
 
Acha kudanganyika kwa nukuu nyepesi, lugha inabaki kuwa na sehemu kubwa sana katika ufundishaji wa kitu chochote kile. Pep Guardiola alijifunza Kijerumani kabla ya kutambulishwa rasmi, nimemaliza kusoma kitabu cha Zlatan Ibrahimovic ambapo anasema Mourinho alijifunza Kiitaliano kwa wiki tatu kabla ya kujiunga na Inter Milan. Mifano ipo mingi sana...Lugha ni chombo muhimu sana katika mawasiliano. Mpira ni zaidi ya kuamrisha watu kukimbia, kukaba na kupanda.
 
Kibadeni anaongea lugha gani? Unaweza kuniambia mafanikio aliyo yapata tangu akabidhiwe jukumu la kuinoa Simba? Acheni story zenu zakwenye kahawa bhana.
 
Mkuu fuatilia soka duniani kote utagundua kuwa lugha sio kikwazo hata kidogo. Bahati njema kocha mpya wa Azam leo amenukuliwa na Mwanaspoti gazeti anaulizwa kuhusu lugha ametoa jibu kama nililoeleza jana kuwa Soka lina lugha yake moja tu duniani kote na hata wakutane mreno na mwingereza, wataelewana tu inapofikia kuwa wanafundishana soka. Lugha haijawahi kuwa kikwazo mahala popote duniani katika kufundisha soka mkuu.

Hapana hii nakukatalia kaka, nchi za wenzetu kocha ni lazima ajue lugha ya nchi anayofundishia timu, kwa hiyo lugha ni kikwazo pia.

Mfano kama umesikia makocha wakihojiwa na waandishi wa habari, huwezi kukuta eti Muitaliano anayeifundisha timu ya Uingereza anaongea kiitaliano, ni kiinglish tu. Bora mchezaji asijue lugha lakini kocha ni lazima.
 
Kibadeni anaongea lugha gani? Unaweza kuniambia mafanikio aliyo yapata tangu akabidhiwe jukumu la kuinoa Simba? Acheni story zenu zakwenye kahawa bhana.
Jaribu kuelewa mada...tunazungumzia umuhimu wa lugha kwenye ufundishaji wa mpira.Hatuongelei Azam, Simba wala Yanga. Acha vichekesho unataka nikutajie mafaniko ya Kibadeni wakati hata ligi haijaisha na hakuna kombe lingine wala mashindano yoyote aliyoshiriki zaidi ya ligi ambayo kafungwa mechi moja...Unaweza kutaja mafaniko ya Brandts, Mwambusi au Hall?
 
Naamini bodi ua uendeshaji ya Azam wamefanya utafiti wa kina kabla ya kufanya maamuzi haya ya kuchukua kocha mpya mwenye CV kubwa lakini asiyefahamu kiingereza wala kiswahili. Sitaki kuamini hawakujadili hili.

Na uzuri lugha ni kitu ambacho mtu yeyote anaweza kujifunza na kumudu mawasiliano kwa haraka tu. Ngoja tuone mwisho wa ligi ndio tutajua pumba na mchele.
 
Jaribu kuelewa mada...tunazungumzia umuhimu wa lugha kwenye ufundishaji wa mpira.Hatuongelei Azam, Simba wala Yanga. Acha vichekesho unataka nikutajie mafaniko ya Kibadeni wakati hata ligi haijaisha na hakuna kombe lingine wala mashindano yoyote aliyoshiriki zaidi ya ligi ambayo kafungwa mechi moja...Unaweza kutaja mafaniko ya Brandts, Mwambusi au Hall?
Umenena mkuu.
 
Hapana hii nakukatalia kaka, nchi za wenzetu kocha ni lazima ajue lugha ya nchi anayofundishia timu, kwa hiyo lugha ni kikwazo pia.

Mfano kama umesikia makocha wakihojiwa na waandishi wa habari, huwezi kukuta eti Muitaliano anayeifundisha timu ya Uingereza anaongea kiitaliano, ni kiinglish tu. Bora mchezaji asijue lugha lakini kocha ni lazima.
Mkuu umenena vilivyo, tatizo la baadhi yetu ni kuangalia tu mechi kwenye TV bila ya kuingia ndani kuchimbua mambo kwa undani zaidi.
 
Mleta UZI atakua mnazi wa Yanga, hana lolote.
Sio hivo mkuu, hapa sijaongelea Mnyama wala Mwananchi. Naongelea lugha kwa ajili ya mawasiliano ya moja kwa moja kati ya kocha na wachezaji.
 
Nimemsikia msemaji wa Azam kupitia RFA kuwa:-
1. Kocha waliyemuajiri ni kutokana na uongozi wa klabu na sio mashabiki, hilo ni sawa lakini hakuna timu isiyokuwa na masabiki hata vilabu vya Simba (mnyama) na Yanga (mwananchi) vilianza kama vikundi tu vya watu wachache na leo pana mashabiki lukuki si ndani ya nchi pekee hata nje ya nchi hii.
2. Mafanikio ya kocha huyu alipokuwa na FC Leopard ni tofauti kabisa na atakavo kuwa na Azam kwa sababu ya lugha. Lugha ni kitu muhimu mno katika maisha ya binadam hivo kwa kuwa huyu hajui Kiingereza wala Kiswahili pana tatizo hapo. FC Bayern Munich walipomuajiri Pep walihakikisha anaifahamu vema lugha ya Kijerumani kwanza na ndipo wakamkabidhi timu, kumbuka Pep ni Mhispania. Sasa huyu kocha hajafundishwa Kiswahili na kama ujuavyo sie lugha ya Kiingereza hatukijui sawasawa itakuwaje?
Sitegemei mabadiliko ya haraka hapo Azam kama ndoto za viongozi wake zinavowatuma.

mawasiliano ni kitu muhimu sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom