Azam FC yatwaa Ubingwa wa kombe la Mapinduzi 2017 baada ya kuifunga Simba SC 1-0

Asubuhi hii nimeenda dukani kwa jamaa kavaa jezi ya SIMBA.. nikamwambia naomba UNGA WA NGANO chapa AZAM KILO 1 nataka nikapike chapati,
Naona kafunga Duka katoka zake hajanisemesha...
Nahisi kenda kuchukua MIZANI YA KUPIMIA.

[HASHTAG]#AZAM[/HASHTAG]..Bidhaa bora ya Bakhresa
 
Simba mlikuwa mnafanya nn zanzbar
Bingwa AZAM
KIPA BORA MANURA AZAM
MFUNGAJI BORA MSUVA YANGA

SASA SIMBA MLIKUWA MNAFANYA nini?
 
1 Azam bingwa karudi na kombe na million 10 medal, 2 Simba karudi na million 5 na medal, 3 Yanga karudi na 4G+4G =8G
 
Hivi jamani tuwe wakweli katika hilo kwani:
Maji tuliyokunywa yao.........
Juice tuliokunywa yao......
TV wanaonyesha wao.......
Watangazaji wao..........
Mpira wameonyesha wao.......
Boti tuliyopanda yao.........
SASA mlitaka tuwafunge AZAM turudi Dar kwa Miguu!!!????
TUACHENI BHANA!!!!!!!!!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
f063858741c4a6c7a06f425ea6890ec5.jpg
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Tangu mapinduzi ianze ndo nimeshuhudia soka safi jana ingawa mimi simba nilikubali kiroho safi kabisa kuwa tumefungwa na kwa mpira wa jana ilikuwa halali yanga ale 4. Na kama mpira ungekuwa unachezwa hivyo timu zote za ligi kuu hata timu yetu ya taifa ingekuwa moto maana sikuona hata mipira mingi ya kubutua ilikuwa kampa kampa tena duh hadi raha.
 
Maji tumekunywa yao......
Juice tumekunywa yao.......
TV wanaonesha wao.......
Watangazaji ni wao..
Mpira wameonesha wao.....
Boti tutapanda lao...

Mlitaka tuwafunge AZAM turudi Dar kwa MIGUU???
Tuacheni bhana...!
 
Ni fainali ya kihistoria leo
Simba sport Club vs Azam Football Club
Mahali: Uwanja wa Amani
Tarehe: 13 Jan 2017 Saa 2:15 Usiku


=> Azam FC mabingwa wa kombe la Mapinduzi 2017 baada ya kuifunga Simba SC.

13' Himid Mao anapiga shuti kali kutoka nje ya 18 na kumshinda mlinda mlango wa Simba, Azam 1-0 Simba
Hongera sana AZAM,naamini mlitumia nafasi muliyoipata vizuri.Simba,tumepambana lakini bahati haikuwa kwetu.
 
Back
Top Bottom