Azam FC imewatimua makocha wake wote raia wa Hispania

PROSPER 05

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
226
217
Uongozi wa Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati AZAM FC Leo Limesimamisha Benchi zima la ufundi la Timu hiyo linaloongozwa na Kocha mkuu Mhispania Zeben Hernandez kutokana na Mwenendo mbovu wa Timu.

Wakati huu ambapo uongozi wa Azam FC upo katika mchakato wa kusaka kocha mpya, kikosi hicho kitakuwa chini ya makocha wa timu ya vijana ya timu hiyo, Idd Cheche na Kocha wa Makipa, Idd Abubakar, ambao walianza kazi jana jioni kukiandaa kikosi kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons.


Azam FC inapenda kuwaambia mashabiki wake kuwa wawe watulivu katika kipindi hiki kwani uongozi umefanya uamuzi sahihi kwa ajili ya kuinyanyua timu juu ili hatimaye ushiriki wetu wa michuano mbalimbali uweze kuwa ni wa kiwango cha juu tofauti na hali ilivyokuwa sasa.


Hernandez anaondoka Azam FC akiwa ameingoza timu hiyo kwenye mechi 18 rasmi ambazo ni za mashindano, 17 za ligi na moja ya Ngao ya Jamii, amefanikiwa kushinda mechi nane, sare sita na kufungwa mara nne.
source AZAM TWO


My Take: Ni jambo zuri Kwani kwa Uwekezaji ule Haiwezekani Wapinzani wetu wawe Stendi, Majimaji, Mbao nk.
Nafikiri sasa Watumie Mechi za Mapinduzi kama Pre-Season kwa ajili ya FA ili kumantain Uwakilishi wa Kimataifa, Ligi kuu kwa sasa ni kama Tumechelewa


=====

Azam FC imemtimua Kocha wake Mkuu, Zeben Hernandez Zeben na makocha wengine raia wa Hispania, wametimuliwa kazi leo baada ya Azam FC kwenda mwendo wa kusuasua.

Azam FC iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 17.

Katika mechi 17 za Ligi Kuu Bara, Azam FC imechinda mechi saba, imepoteza nne na sare sita, hali ambayo wazi inaonekana kutoufurahisha uongozi wa Azam FC hata kidogo.
 
Uongozi wa Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati AZAM FC Leo Limesimamisha Benchi zima la ufundi la Timu hiyo linaloongozwa na Kocha mkuu Mhispania Zeben Hernandez kutokana na Mwenendo mbovu wa Timu
source AZAM TWO

My Take: Ni jambo zuri Kwani kwa Uwekezaji ule Haiwezekani Wapinzani wetu wawe Stendi, Majimaji, Mbao nk.
Nafikiri sasa Watumie Mechi za Mapinduzi kama Pre-Season kwa ajili ya FA ili kumantain Uwakilishi wa Kimataifa, Ligi kuu kwa sasa ni kama Tumechelewa
Tanzania hatuna uvumilivu ngoja watimuliwe tu
 
Back
Top Bottom