Azam FC haikuonyesha professionalism kwa Sure Boy

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,307
12,602
Mpira wetu ni semi- professional, yaani bado ni vuluvulu. Kumzuia mchezaji anayetaka kuondoka hakuisaidii club wala mchezaji. Kama akicheza chini ya kiwango kwenye club yako majibu utakuwa nayo tayari hata kama sababu siyo hiyo.
 
kavulata,

Wapi Sure Boy alisema anataka kuhama au wewe unasikiliza tu hawa waandishi wa mlungula? Jana ulimsikia mwenyewe akisema hana mpango wa kuhama alafu wewe unakuja na singeli zako.
 
Kwani mkataba wake umeisha?

Kama umeisha yanga wakae mezani na azam wazungumze acheni janja janja. Kumfuata mchezaji mwenyewe wakati ana mkataba ni kupoteza muda

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
kavulata,
Yanga bwana, wameandika barua inayoonyesha kwamba Sure Boy ndio ameandika kuomba kuondoka Azam, halafu wakampa mesenja aipeleke, ina tarehe ya kesho yake.

Sure Boy ameikana barua kwamba wala yeye hajaandika, na wala hata haieleweki kwa nini Yanga waandike barua kwa niaba ya mtu mwingine!

Ila nahisi mesenja hakuelewa, labda aliambiwa ampelekee Sure Boy, yeye akaipeleka ofisini 😁😁😁
 
kavulata,

Hakuna vya dezo mmetajiwa dau mkafeli sasa nini kimezuiwa hapo? Unakumbuka ishu ya PC kati ya liver na Barca? Unajua liver walikunja mkwanja kiasi gani?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom