AYOTV VIDEO: Maamuzi ya Mahakama Arusha kuhusu kesi ya aliyekuwa Mwenyekiti UVCCM

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
kkkkkkkkkk.jpg

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo April 28, 2017 imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, Lengai Ole Sabaya ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya kughushi na kutumia kitambulisho cha Usalama wa Taifa.

Hakimu Gwanta Mwankuga ambaye alikuwa anasikiliza kesi hiyo, amesema upande wa Jamhuri umeshindwa kupeleka mashahidi katika kesi hiyo na kusema Mahakama haijamuachia huru mshtakiwa kwa ombi la Jamhuri kutaka kuondoa shitaka hilo Mahakamani, bali amemuachia kwa kifungu cha sheria namba 225 kipengele cha 5.

Ayo TV na millardayo.com imempata Charles Abraham ambaye ni Wakili wa Lengai Ole Sabaya na hapa anafafanua zaidi kuhusu kesi hiyo.
Bonyeza LINK HIYO kutazama…
VIDEO: Maamuzi ya Mahakama Arusha kuhusu kesi ya aliyekuwa Mwenyekiti UVCCM - millardayo.com
 
Back
Top Bottom