Awezaye kutabiri aniambie miaka 10 ya Mhe magufuli Tanzania itakuwa wapi??

mkafrend

JF-Expert Member
May 12, 2014
3,053
2,000
Nchi kuendelea kiutamaduni, kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia huwa ni mchakato.

Sasa wale mnaoweza KUTABIRI nijuzeni miaka ya utawala wa Mhe. JPM TANZANIA Itakuwa wapi??

1. Tutakuwa na maendeleo ya kisiasa zaidi ya watangulizi wake??

2. Tutakuwa na maendeleo ya kiuchumi - zaidi ya tulivyo sasa?? -

3. Tanzania itakuwa na watu wenye mshikamano na umoja kama ikivyokuwa wakati wa Nyerere??

4. Nchini Zanzibar (Pemba na Unguja) watashirikiana kabisa na kuwa kitu kimoja?

WATANZANIA TUMWOMBEE MAGUFULI ILI ATAWALIWE NA HEKIMA KILA AAMUWAPO JAMBO AKIWA RAIS WA NCHI.

VISASI KAMWE VISIWEPO KWA KUNDI LOLOTE LILILOMPINGA, LINALOMPINGA NA LITAKALOMPINGA MBELENI.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
25,815
2,000
Huwezi kujua yakesho kwani wewe mungu?
Mambo yakutabiri mwisho kwenye mipira
Lakini kwa nchi hilo analijua mungu tu.
Hapa nikuzidisha maombi kwa Rais wetu mwenyezi mungu azidi kumlinda na kuumpa nguvu zaidi.
 

expedition

JF-Expert Member
Jul 16, 2016
690
1,000
1. Siasa ya upinzani itadorola japo CCM itaendelea kuwa na nguvu.
2. wananchi tutaheshimiana
3. vijana tutapata tu mawazo ya kujiajiri kutokana na serikali kubana ajira.
4. Serikali itakuwa na uchumi imara.
5. wananchi tutakuwa na nidhamu ya fedha.
6. Na mimi nitagombea ubunge jimbo fulani ivi na nitashinda ikibidi kwa kutumia njia iliyompa ushindi Trumph.
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
10,610
2,000
BINAFSI NAMWOMBEA "HEKIMA"siombi lolote zaidi ya hilo,aione hii ni Tanzania,ina kusini magharibi,kusi na kaskazi na kote wanahitaji maendeleo na hali bora zaidi.
Afahamu nchi hii ina dini nyingi nyingi,na zote zinataka haki,usawa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom