Aweso aridhishwa na utekelezaji wa mradi wa zaidi ya bilioni 23 Morogoro vijijini

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
664
829
Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb), ameridhishwa na utekelwzaji wa Mradi wa Maji wa Morong’anya unatekelezwa na RUWASA Morogoro Vijijini.

Mradi wa Maji Morong’anya ni miongoni mwa miradi mikubwa 2 ya maji iliyosanifiwa na watumishi wa RUWASA na inayoendelea kutekelezwa na ofisi ya Meneja RUWASA Wilaya ya Morogoro kupitia fedha za Mfuko wa Maji.

Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi Kampuni ya M/S EMIRATE BUILDERS CO. LTD ya Mkoani Dar es Salaam kwa gharama ya shilingi 23,186,021,991.

Utekelezaji wa mradi huu ulianza tarehe 24/03/2022 na unatarajiwa kukamilika tarehe 23/03/2023, kwa mujibu wa mkataba.

Mradi utahudumia Vijiji 19 kwenye Kata 7 za Mikese, Kibuko, Tegetero, Kinole, Mkuyuni, Gwata na Tomondo.

Chanzo cha maji cha mradi huu ni Mto Mbezi uliopo Kata ya Tegetero wenye uwezo wa kuzalisha maji lita 4,449,600 kwa siku wakati mahitaji ya maji kwa sasa ni lita 1,600,000 kwa siku.

Mradi huu ukikamilika utatoa huduma bora za maji kwa wananchi wapatao 52,000 kwenye vijiji hivyo.
 

Attachments

  • IMG-20230104-WA0210.jpg
    IMG-20230104-WA0210.jpg
    101.8 KB · Views: 3
  • IMG-20230104-WA0220.jpg
    IMG-20230104-WA0220.jpg
    99.9 KB · Views: 3
  • IMG-20230104-WA0216.jpg
    IMG-20230104-WA0216.jpg
    144.1 KB · Views: 4
  • IMG-20230104-WA0213.jpg
    IMG-20230104-WA0213.jpg
    99.3 KB · Views: 4
Back
Top Bottom