Awaua watu 14 wa familia yake nchini India

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Mwanamume mmoja nchini India amewachoma kisu na kuwaua watu 14 wa familia yake wakiwemo wazazi wake walipokuwa wamelala.

7 miongoni mwao walikuwa watoto.

Polisi walisema kuwa waliitwa katika nyumba moja katika kijiji cha Thane, karibu na Mumbai na majirani waliomsikia mwanamke akipiga kamsa akitaka asaidiwe.

Mwanamke huyo, ambaye ni dada ya muuaji, alikuwa wa pekee katika familia hiyo kunusurika mauaji hayo ya kikatili.

Maafisa wa upelelezi wanasema inaokana kuwa mtu huyo alifunga milango yote kwa ndani kabla ya kuwaua jamaa zake.

Kisha alijitia kitanzi.

Wachunguzi wanaamini mauaji hayo yalitokana na ugomvi kuhusiana na urithi.

Hasnin Warekar mwenye umri wa miaka 35 inaaminika kuwa aliweka dawa ya kulala katika chakula cha jioni alipokuwa akipanga njama hiyo ya kikatili.

Aliwaua kwa kuwachinja.

Warekar alikuwa ni mhasibu mjini Mumbai.


Chanzo:
BBC
 
Back
Top Bottom