Award Verification Number (AVN) zinazotolewa na NACTE

Arch.katunzi

JF-Expert Member
Sep 18, 2014
250
143
Kwa wale wahitimu wa diploma ambao hatujapata AVN kutoka NACTE kutokana na vyuo kuchelewa ku upload matokeo ya diploma kwenye system ya NACTE. System ya Ku upload matokeo NACTE, itafunguliwa tar.15/09/2020 kwa mujibu wa calendar yao. Na TCU wanaanza udahili wa vyuo tar. 31/08/2020, kwa mujibu wa calendar.

Kwa wale mliopitia njia hii kuna uwezekano wa kupata AVN on time ili kufanya application za vyuo kwa mwaka huu?Mbinu gani itumike ili kupata AVN mapema baada ya kufunguliwa system za NACTE kuruhusu vyuo ku upload matokeo kwenye mfumo?

Ushauri wenu ni muhimu sana ili tuweze kupata uhalali wa ku join bachelor degree kwa mwaka huu.
 
Tatizo ni vyuo vyetu,hawatimizi wajibu wao.Hawakubari kabisa kufuata muongozo wa NACTE unao vitaka vyuo ku upload matokeo ya kila mwisho wa semester katika system ili yawe verified na balaza.Wanasubiri mwisho kabisa umehitimu,ili uanze kusuguana nao...!

Lakini pia NACTE wameshindwa kusimamia agizo lao kwa vyuo.Nadhani kama hili swala lingetungiwa sheria ambayo kama vyuo vitachelewa ku upload matokeo ya wanafunzi ya kila semester bila sababu ya msingi,basi vichukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kutozwa faini za mamilioni ya shilingi.Kwa style hii hakuna chuo kitaleta mzaa wa kupoteza muda wa watu...!Maana mpaka sasa cna hakika kama mwaka huu nitaweza kuendelea na bachelor degree. Vyeti vyangu vyote vya diploma niko navyo still bila AVN sina sifa ya kuendelea na masomo ngazi ya degree...!
 
Dirisha LA kutuma matokeo linafunguliwa sept 15 hvyo ongea na chuo ili wakutumie... Fanya maneno na coordinator wako atume chapu
 
Kutokana na TCU kufungua mapema dirisha la udahili wa vyuo,na necta kutangaza matokeo ya kidato cha sita mapema..

Kwa nini nacte wasione umuhimu wa kufungua system zao mapema,kuruhusu vyuo vya kati ku upload matokeo ya diploma ili zoezi la kupata AVN liendane na muda uliyowekwa na TCU wa kuomba vyuo.

Nimeangalia pia calendar ya TCU,naona mwaka huu wana round nne peke yake za kutuma maombi ya chuo.Siyo kama mwaka jana ambapo walikuwa na round nne.Nacte namba zao za simu ni mapambo tu,hazipatikano muda wote,na zile zinazopatikana,hazipokelewi hata ukipiga cku nzima.

Naamini jukwaa hili ni kubwa,wapo wahusika wa hiki chombo (NACTE),salamu hizi wazipate wajue jinsi ya kutusaidia.

Kwa mbele chombo hiki kiangalie jinsi ya kuviwajibisha vyuo ambavyo kwa sababu zao nyepesi na zisizo eleweka,vinachelewesha kwa makusudi ku upload matokeo ya wanafunzi katika mfumo wa nacte mapema ili iwe rahisi kwa wahitimu ku process avn zao mapema.

Nawasilisha...!
Hebu nikusahihishe hapo.. Mwaka huu TCU inaonesha kuwa watakuwa na round mbili tu na ya kwanza ndo hii iliyofunguliwa ita-take place kama siku 30 then itafungwa
 
Hebu nikusahihishe hapo.. Mwaka huu TCU inaonesha kuwa watakuwa na round mbili tu na ya kwanza ndo hii iliyofunguliwa ita-take place kama siku 30 then itafungwa
Shukrani kwa kunisahihisha,...!Mwaka huu ni round mbili kwa mujibu wa calendar ya TCU.

Typing error, nimerekebisha mkuu...!
 
Helo .msaada kwenye Transcript na 3.6 GPA
NIMEFANYA application na jaza AVN yangu kwenye Application ya muhimbili inaleta 2.6 GPA #MSAAAAADA JAMAN
Hii kitu imekuwa ikisumbua sana,hapo wasiliana na chuo ulicho soma diploma yako...!
 
Back
Top Bottom