Nyakageni
JF-Expert Member
- Feb 1, 2011
- 15,046
- 5,092
Hatujapata mapendekezo ya upande wa serikali ili tupime uzuri na ubaya wa maoni yake. Ni vigumu kutolea maamuzi kwa maoni ya upande mmoja. Ikumbukwe kuwa mgogoro ni wa pande mbili: Serikali na Madaktari. Upande wa madaktari hauwezi kuwa HAKIMU kwa shauri lake yenyewe. Madaktari hawawezi kusema kwa uhakika kuwa Serikali imekosa hiki au kile, jambo hili kwa maoni yangu haliwezi kuwa sawa.
Madaktari wamekuwa wakisisitiza kutaka kugoma kila mara, lakini jamii na maadili ya taaluma ya udaktari yana wazuia. Hivyo kila wakipata kisingizio cha aina yoyote wanahamaki kutaka kutimiza azma yao ya kutaka kumuumiza bila huruma mlalahoi mnyonge. Hii haikubaliki hata kidogo kama malaria. Madaktari mnatuonea bure sisi wanyonge huku mkiwa tayari mlikula fedha zetu kwa kuwasomesha. Hawa mnaodhani mnawaadhibu hawapati adhabu hiyo. Lakini pia uchumi wetu bado ni mdogo, ikiwa Viongozi wanaonekana kufuja mali isivyohalali isiwe kigezo cha kudai zaidi hata ya uwezo halisi wa nchi. Hata leo hii tukimteua mwiungoni mwenu Daktari mmoja aende Ikulu hataweza kuwalipa madaktari kadri ya madai yao. Nakubaliana maslahi ya madaktari yanaweza kuboreshwa, lakini uboreshaji ni mchakato, huwezi kuboresha maslahi kwa usiku mmoja.
mkuu hilo linawezekana kabisa. Almasi za Mwadui tu zinatosha, pipi moja mil 800! Tafakari