Awamu ya tano Tanesco hawakukarabati miundombinu ya umeme, sasa mmehitimisha ukarabati tusikie mgao tena

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Mmnetangaza wenyewe kuwa mmehitimisha ukarabati wa miundo mbinu ili umeme upatikane vizuri. Tunataka tusisikie habari ya mgao na umeme kukatika katika hovyo imeisha kama enzi za awamu ya tano.

20220211_025144.jpg
 
Mgao hautakoma ila sababu ya mgao itabadilika
Mpaka sasa Wana draft letter zenye sababu Kama 1000 its a matter ya kuchagua ni siku ya mvua waseme miundombinu imepigwa radio au upepo mkali, au jua Kali, au kelele zimezodi, sauti zipungue , ndugai amejiuzulu, Yani basi tu japo watukere tu 😃
 
Mmnetangaza wenyewe kuwa mmehitimisha ukarabati wa miundo mbinu ili umeme upatikane vizuri. Tunataka tusisikie habari ya mgao na umeme kukatika katika hovyo imeisha kama enzi za awamu ya tano.

View attachment 2115389
Itapungua miundo mbona zamani sana inabidi periodic maitanance tuache siasa kwenye mambo ufundi
 
Ivi watu hawawezi kuchangia hoja bila kutaja ccm au chadema
 
Kati ya mambo ninayopinga ni huo uongo kwamba hakuna ukarabati uliofanyika awamu ya tano, unaotumika kuhalalisha kuondolewa kwa waziri wa nishati na kutenguliwa kwa mkurugenzi wa Tanesco. Wenye macho wanaona kuwa miradi ya kinyerezi, mradi wa miligoti ya concrete, umeme wa REA pamoja na miradi mingine mingi iliibuliwa nakutekelezwa awamu ya tano.

Kama lengo nikurudusha fadhila kwa wazee wa CCM kwa kuwapa vyeo watoto wao, basi itumike njia nyingine pasipo kuwavunjiwa wengine heshima yao na legacy yao.

Nasikia kuna mradi mkubwa tu uliobuniwa awamu ya tano wakutengeneza nguzo za high tension za chuma na shirika moja la umma na uko mbioni kukamilika.

Jitihada ni nyingi na hazipimiki tuache upotoshaji kwenye haki toeni haki
 
Daraja la TANZANITE anasifiwa bibi ushungi, yaani ni mambo ya ajabu sn
 
nani kakwambia miundo mbinu hii ya Tanesco iliyooza inaweza kukarabatiwa kwa 10days...

Tanesco wanahitaji mwaka mmoja kukarabati miundo mbinu yao iendane na mahitaji.
Wanapaswa kuwa na plan tu ya kazi ili kusiwe na mgao wa moja kwa moja bali kuwe na ukatikaji kidogokidogo huku wakifanya hizo repair..
 
Tokea naifahamu Tanzania umeme haujawahi kuacha kukatika.

Kila awamu na siasa zake ila nia ya kutatua tatizo imebakia kwa kudra za Mungu tu.

Kuna ka syndicate katakua kapo na kananufaika sana na tatizo hili.

Ni vyema kwa maslahi mapana ya nchi kakatafutwa mizizi yake na kuing'oa kabisa.
 
Back
Top Bottom