Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,830
- 976
Wanajamvi, salaam.
Moja ya Jambo muhimu na la lazima ni serikali kuhakikisha inawalinda raia wake kwa gharama yoyote ile. Moja ya sababu kubwa ya vifo nchini Tanzania ni vile vitokanavyo na ajali za barabarani. Aidha ajali hizo zimesababisha ulemavu na kuongeza idadi ya mayatima nchini kwetu. Vijana hasa bodaboda, waenda kwa miguu, madereva na abiria wengi wamepotea. WHO inasema idadi ya vijana wanaokufa kwa ajali za barabarani inazidi ile ya wanaokufa kwa virusi vya UKIMWI. Hii haikubaliki.
Miongoni mwa mambo yanayotajwa kupelekea ajali hizo ni pamoja na mwendokasi, ubovu wa vyombo vya usafiri, kukosa umakini miongoni mwa madereva na watumiaji wengine wa barabara, madereva wasiopata mafunzo na ubovu wa miundombinu.
Sisi wote ni mashahidi wa jinsi serikali ya awamu ya tano ilivyojitahidi kuhakikisha inaokoa maisha ya raia wake kwa kutekeleza mambo ambayo ni muhimu katika kuzuia ajali za barabarani.
¹ Miundombinu ya barabara na madaraja imejengwa na inaendelea kujengwa nchi nzima. KWELI AU SI KWELI?
² Usimamiaji mzuri wa sheria za barabarani. Tochi, faini, elimu kwa madereva, abiria na watumiaji wa barabara. Ukiwa kwenye mabasi mara kwa mara vipande vya video vya elimu kwa umma kutoka mamlaka husika huchezwa. Namba za simu za RTO's zimebandikwa kwenye mabasi. KWELI AU SI KWELI?
³ Upigwaji marufuku wa viroba. Hivi vilihusika sana kwa ajali za bodaboda. KWELI AU SI KWELI?
Nimetaja mambo machache sana, Ila ningefurahi mkiniongezea hatua nyingine zilizochukuliwa na serikali.
Je, kwa hatua hizo, ajali zimepungua au hazijapungua?
Kama zimepungua, je hili sio jambo la kupongeza?
Je, kuna Jambo kubwa zaidi ya kulinda uhai wa watu wako?
#Amani on Monday night