Awamu ya tano na dhana ya ukusanyaji kodi

DNR

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
523
337
Habari za weekend wanaJF,

Ukusanyaji wa kodi ni jambo zuri hakuna anae pinga lakini huu ukusanyaji wa awamu ya tano ni kama unaelekea kutubana sana wananchi hasa wa hali ya chini maana nguvu inayotumika na maongezeko ya kodi mbali mbali ya bajeti hii yanatia shaka uwezo wa kiutendaji mfano kuna kodi nyingine kama za pango zilikuwepo ila watu mpaka walishasahau kama ipo yaani siku hizi ni kodi kodi kodi kila muda

Maswali yanakuja:-
1. Kukusanya kodi ndio njia pekee ya kuingiza kipato serikalini?
2. Je kuwakamua wananchi ndio njia pekee awamu ya tano ya Kuingizia serikali Mapato?
3.Ni vyanzo vipi serikali inaweza tumia mbadala ili wafute baadhi ya kodi?
 
Wameweka kodi kubwa kwenye nguo na viatu vya mtumba ili kulinda viwanda vya ndani. Sasa jiulize, hapa Tanzania kuna viwanda vinavyotengeneza viatu zaidi ya kile cha Bora pale Nyerere Road ambacho kinatengeneza kandambili aina ya Yeboyebo? Viwanda vya nguo navyo ni vile vya wachina vinavyotengeneza jezi zile zinazomwagwa chini pale Shule ya Uhuru. Watanzania walio wengi ni wale wanaotumia nguo za mitumba, kwahiyo unapozidisha kodi kwenye nguo hizo ina maana unawakomoa watanzania.
 
Back
Top Bottom