Safari hii tulianza kwa matumaini makubwa sana, tulianza kwa kusherekea utumbuaji wa majipu, hasa tukianzia pale Bandarini. Hii iliamsha shamra shamra kila mahali, ghafla tulimsahau JK.
Ndani ya miezi sita mambo yamegeuka ghafla, tukiwa na tumaini la nafuu ya maisha kinyume chake walala hoi tunaambulia machungu yasiyo kifani.
Nauli ya daladala Mbezi, posta, Kariakoo tulizoea shs mia sita. Leo hii nauli ni mia sita hamsini hadi elfu moja na hamsini. kwa maana ya kutoka Mbezi kimara shs 400, Kimara posta, Kariakoo 650.
Walalahoi angalau kwa shs elfu 3000 watoto wetu waliweza kunywa chai, kwa maana kilo ya sukari shs 1800 na mihogo ya elfu moja. Leo hii Sukari tu shs 2800 mpka 3200 kwa Dar es Salaam, Maeneo ya Mbezi mwisho, lakini kuipata unaweza tumia zaidi ya siku mbili ukitafuta kilo ya sukari.
Watoto wa walalahoi kwa kutambua shida kwenye familia zao wakakimbilia UDOM kusoma diploma ya ualimu kwa vile waliahidiwa mkopo, wakitarajia mkopo utawasaidia hata nyumbani. Kwani kibanda alichotumia mama kwa biashara yake kimevunjwa, Nyumba ya kuishi imevunjwa kwa kuwa imejengwa bondeni, Chuo nako wamefukuzwa kwa kuwa ni vilaza. Ni vilaza kwa sababu ya ufukara wao, ni vilaza kwa sababu wametoka shule za kata.
Baba alikuwa anafanya kazi kwa mwekazeji amesimamishwa kazi ana miak 45 PPF, NSSF wanasema asubiri miaka 55 ama asaini waraka wakujifunga kuwa hatoajiriwa kwa kipindi cha maisha yake. Nani Mkombozi wa kundi hili?
Walionekana kuwa watetezi wa huyu mlalahoi Bungeni wanaambiwa mwaka huu wote hakuna kukanyaga? Tanzania , Tanzania ina wenyewe na wenyewe wako vyuoni wakiwa na division four point 30 na mikopo asilimia mia moja,
Tanzania ina wenyewe na wenyewe wanaweza kuitwa ma DKT wa falsafa ili hali wana degree moja. Tanzania ina wenyewe na wenyewe wanaweza kupata masters wakiwa na certificate, Tanzania ina wenyewe na wenyewe wanaweza kusoma A level hata chuo cha ualimu Butimba.
Tanzania ya Wadanganyika,