Awamu ya Tano iliua UDART, hili tuliseme wazi si kumung'unya maneno

Acha kupotosha wewe,

Ukweli ni kwamba huyo marehemu ndiye alikuwa anapiga. Ubabe wake ulikuwa ni zuga tu na uhuni wake. Marehemu amepiga hela ndefu Sana mfano alitumia 1.2 trillion kununua ndege by cash ambapo alilipwa 10% ya hiyo hela ,unafikiri ni sh ngapi?

Yeye alikuwa ni mwizi Namba 1 wa nchi hii.

Usijifanye hujui wakati unajua acha kudemka.

angekuwa mpigaji kwa miaka aliyokaa wizara ya ujenzi angekuwa tajiri kuliko bakhresa au mo

kusema kwa msisitizo, kwa hasira kwa namna yoyote hakumfanyi yeye kuwa mpigaji

wizara inayopitisha hela nyingi TZ ni ujenzi na unayemsema anafanyia nini??

acha uongo wa kukupa faraja, wewe bado maskini na jikwamue, usitafute visingizio🤣🤣🤣
 
Lakini hao wote si ndio Wazalendo waliowekwa na JPM.

Ccm uzalendo lazima uwe fisadi.😅😅😅
Rais hawezi kusimamia kila kitu, mpaka pen maofisi au sindano mahospitali. Mh. Spika juzi kasema, vijana wa kitanzania bila kuiba hawana raha moyoni, mradi huu, unafilisiwa na watu walioaminiwa na wala sio tax holiday au uwekezaji.

Kumbuka bado kuna mabasi 100 yanazurula mitaani, lakini mapato yake yanaishia mifukoni kwa wale wanaojiita watoto wa mjini.
 
angekuwa mpigaji kwa miaka aliyokaa wizara ya ujenzi angekuwa tajiri kuliko bakhresa au mo

kusema kwa msisitizo, kwa hasira kwa namna yeyite hakumfanyi yeye kuwa mpigaji

wizara inayopitisha hela nyingi TZ ni ujenzi na unayemsema anafanyia nini??

acha uongo wa kukupa faraja, wewe bado maskini na jikwamue, usitafute visingizio🤣🤣🤣
Wazalendo wa magufuli kila mahali wameiba. Sisi wasaliti wa mabeberu tunacheka tu😅😅
 
Uache siasa za changa la macho, Serikali ya JPM ndiyo imeua utendaji wa UDART.

Barabara za UDART kweli ni mali ya serikali lakini mradi wa mabasi mwendo kasi ulikuwa toka mwanzo ni mradi binafsi (private investment) uliowekezwa na mtanzania, Nd Kisenha.

Serikali ilifanya kila njia kumnyima pumzi mwekezaji huyu wa UDART. Alipoagiza mabasi alinyimwa katakata kuyatoa bandarini mpaka hela yote ipatikane kulipa kodi.

Huku ni kukosa ushirikiano kwa muwekezaji, ambapo wale wa kigeni hupewa Tax Holiday au Mkataba maalum kwa malipo ya kodi kubwa.

Hii ingewezesha huduma iendelee, biashara iendelee na kodi ilipwe. Hili ni kosa, maana serikali haikuwa na msaada wowote kwa muwekezaji.

Pili, tunasikia tetesi kuwa sasa UDART ni mali ya Serikali maana baada ya Nd Kusenha kufunguliwa madai ya Uhujumu uchumi, kwawaida ya modus operadi ya Awamu ya 5kwa wafanyabiashara, serikali imejimilikisha uendeshaji.

Serikali zote toka Awamu ya kwanza hadi nafikiri Mwinyi (miaka zaidi ya33) mfupa wa DMT (Dra es Salaam Motor Transport) na UDA (Usafiri Dar es Salaam), ziliwashinda.

Sasa sijui Awamu ya 5 ndio wangeweza Kuendesha UDART?

Mbaya zaidi serikali inaua moyo wa wazalendo kuingia miradi mikubwa kiuwekezaji, kinyume cha wanachoongea majukwaani. Ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa kwa UDART kweli sioni mantiki yake zaidi ya kusema Serikali imachukua na kuanza mradi huu on a false start.

Sana sana ni kujikosha kwa wananchi kwa failures za serikali yenyewe, kusaidia wazalendo kuwekeza nchini mwao.
Ili twende vema tujikumbushe ulipoanza mgogolo na tuone mchango wa Serikali hapa:

"TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 24 Aprili 2018 Ufafanuzi juu ya utoaji wa huduma ya Ticketi za kielektroniki kwenye Mradi wa mabasi ya mwendo kasi.

Kampuni ya Maxcom Africa PLC ni mmoja kati ya wabia wanaoshiriki katika utoaji huduma katika Mradi wa uendeshaji wa Mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar es Salaam, Kazi ambayo ilianza mnamo tarehe 16 Mei 2016 pindi tu Mradi huu ulipozinduliwa katika awamu ya Kipindi cha mpito (Interim period).

Kuanzia tarehe 13 Aprili 2018 kumekua na hali ya sintofahamu katika vituo vya Mwendo kasi, na kumekuwapo na uuzwaji wa tiketi za karatasi (za vishungi) ambazo hazitolewi kwenye mfumo wa Tiketi za Kielektroniki ulioidhinishwa na wasimamizi wa mradi huu (DART Agency), na pia kumekuwapo na nyakati ambazo abiria wanasafirishwa bila kulipa nauli.

Tunaomba ifahamike kwamba haya yanayoendelea yanaratibiwa na kampuni ya UDA-RT ambayo mbia wake mkubwa ni Simon Group ambao wanamiliki mabasi haya ya Mwendokasi. Maxcom Africa PLC waliingia mkataba kutoa huduma ya tiketi za kielektroniki katika mradi huu wa Mwendokasi chini ya kampuni ya UDA-RT kutokana na maagizo yaliyotolewa na serikali.

Kutokana na Mkataba huo Maxcom Africa PLC tuliweka Mifumo, Rasilimali watu, teknolojia na wasimamizi katika mradi huu. Ila katika hali isiyo ya kawaida tangu mradi huu umeanza Kampuni ya UDA-RT imeshindwa kuilipa kampuni ya Maxcom Africa PLC gharama za uendeshaji, uwekezaji na hata stahiki za wafanyakazi (ikiwamo michango ya hifadhi za jamii na tiba) hivyo mnamo Februari 2017 kampuni ya Maxcom Africa PLC tuliamua kufungua kesi ya madai katika Mahakama kuu ya Tanzania, Kesi ambayo mpaka sasa inaendelea kusikilizwa."
UDART.png
 
marehemu POMBE alikuwa anapigwa daily na wajanja aisee nashangaa ule ubabe wake wote lkn bado wahuni wa mjini wamepiga hela ndefu Sana hakika wezi WA nchi hii wanatisha
Kosa kubwa walilofanya ni kutimia mabasi ya kichina, hayana uimara japo yanauzwa kwa bei nafuu
 
hivi, ile sehemu ya kulaza na kushughulikia mabasi ya mwendo kasi, nani alipachagua?

kweli kulikuwa hamna watu wenye ujuzi na systems za GIS wangeweza kuwashauri kuhusu mvua na lile eneo?

hasara ninayo ona kila kukicha ni jinsi gani mabasi yale, mapya kwa zamani, yamekuwa yanaharibika kila mvua ipitapo!

inawezekana palikuwa sehemu sahihi lakini huenda kuna kiasi kilitafunwa ambacho kingetumika kupainua. zaidi ya hapo, kwa kweli sielewi.

hasara za hii nchi, unaweza kumtukana kila raisi aliyepita!
 
marehemu POMBE alikuwa anapigwa daily na wajanja aisee nashangaa ule ubabe wake wote lkn bado wahuni wa mjini wamepiga hela ndefu Sana hakika wezi WA nchi hii wanatisha
Huwezi kukomaa kujiimalisha mtu binafsi, badala ya kuimalisha mifumo!utapigwa tu!china/korea kask, watu wanapiga na kuna sheria ya kunyongwa sembuse hapa ambapo kuna pre bargaining!!yeye alidhania kuwa kuzibiti habari ndio soln!!eti hata watu wakapiga wananchi wasijue?!!wakati anaingia madarakani dart ilikuwa inaenda vizuri, akaja akawapiga chini wale selcom waliokuwa wanakatisha tiketi kwa mfumo wa electronic, akawapa tenda ttcl, wakaanza za vishina!!jana anakuja vp kama vile anashangaaa alikuwa hajui!!??pesa hizo zinazopatikana zinakwenda hazina kurudi ni tabu hayo mabasi yatatengenezwa na nini??
 
Ndio umuhimu wa kusoma na kuelewa mkataba. Unapoweka tender na kaweka bei ya chini ili tu ushinde tender na kutegemea uta negisiate mbeleni, ni wewe ndio itakuja kuumia.

Simon group was a not best fit to run this company, they haven't run any public service company before and their not willing to put down a substantial investment.
Kama Simon hawakuwa kampuni inayokidhi,serikali ilitakiwa kutafuta kampuni nyingine mbadala na kuikabidhi mradi huo.

Hakuna namna serikali kama serikali inaweza kuendesha miradi ya namna hii. Hakuna! Tusidanganyane! Tutaendelea kutesa tu wananchi ambao wanategemea usafiri wa umma.
 
Wewe ukienda hospitali una tatizo linahitaji upasuaji wakikuambia atakayekupasua hana elimu na ujuzi wa upasuaji..utakubali?
Kila fani inahitaji elimu, ujuzi, maarifa na uzoefu ili angalau kuwa na uhakika wa kufanikiwa, Kisena hakuwa na uwezo kurun sekta ya usafirishaji...tuache ubabaishaji na umachinga kwny kila jambo..kifupi hakustahili!
Ni bora hata Kisena alivyokuwa anaendesha. Je hao menejimenti iliyowekwa na serikali wamefanyaje? Umeona madudu yao jana?

Hebu acheni roho mbaya zenu za kuchukua sekta binafsi. Huyo unaembeza ameacha hapo mabasi 140 yaliyokuwa yanatoa huduma na mengine mapya 70 yakiwa bandarini! Hao menejimenti ya serikali wameleta hata basi 1? Hakuna!
 
Ni bora hata Kisena alivyokuwa anaendesha. Je hao menejimenti iliyowekwa na serikali wamefanyaje? Umeona madudu yao jana?

Hebu acheni roho mbaya zenu za kuchukua sekta binafsi. Huyo unaembeza ameacha hapo mabasi 140 yaliyokuwa yanatoa huduma na mengine mapya 70 yakiwa bandarini! Hao menejimenti ya serikali wameleta hata basi 1? Hakuna!
Achana nao hawa mapandikizi ya Burundi! Roho mbaya ndo jadi yao. Wanaua watu wanaofanya vitu vizuri na kutengeneza ajira kwa mamia ya watanzania alafu wanaharibu future za vijana 814 wa jkt waliowaahidi kuwaajiri baada ya kuona hawawezi kuwaajiri. Hizi akili za mshenzi magufuli hazitakiwi kushika tena uongozi wa nchi yetu!
 
unawasaka wewe na nani.
Mtu anafanya biashara vizuri tu, akiweka benki zinatafunwa na TRA.
Akiweka nyumbani money laundering!
Hayo maneno yameshakuwa ni wimbo tu! Kama huna makosa kwa nini usijitetee? Uliwahi sikia Pesa ya Mengi imetafunwa? Pesa ya Dewji imetafunwa? Au utasema wamenyamaza au walinyamaza tu! Wanaojidai misheni tauni watafilisika.
 
Uzuri sisi wengine tupo humu JF kitambo na akili zetu ni zile zile hatuendi na upepo. Soma huu uzi na comments zake alafu umpe JPM heshima yake.


Kila kizazi kinapojiunga na JF kinajifanya kufundisha wengine, kumbe mambo yanaeleweka siku nyingi. Sijaelewa mtu kama Jidu La Mabambasi anawaza nini kuleta utetezi wa kitoto kiasi hiki. Is this all about his/her thinking? Kama ni urafiki na hao wezi, nalo ni jambo la kujiuliza kwamba unawezaje kuwa mtu wa bei ndogo kiasi hiki hadi kutetea wenye akili mbovu kama hao akina Kisena.
 
Hili jambo mimi nilishindwa kabisa kulielewa, vifaa ambavyo vinaenda kusaidia wananchi serikali inagoma kabisa kuvitoa! Sasa walipata faida gani? Kodi hawajapata, wananchi huduma hawajapata. Si wangeweka special agreements, kila siku 50pc ya revenue iende kulipa kodi, how difficult was that! Watanzania hatujui ni namna gani Mungu ametuokoa na lile jitu.

Na huu ujinga wa BRT Phase 1 ndio umetunyima pesa ya Phase II na III, World Bank waligoma kutoa pesa tena. Maana hii ya kwanza tumechemka.
Ninayesoma maadishi kama haya ya kwako, moja kwa moja najua we ni bonge la layman. Yaani serikali ikuruhusu kuchezea mali ya umma kwa wizi kwa kuwa tu unalipa hiyo 50% unayodhani ni pesa nyingi sana! Kama unamiliki boda-boda hiyo ni sawa, endelea, lakini siyo mali ya serikali.
 
40 Reactions
Reply
Back
Top Bottom