Awamu ya Tano iliua UDART, hili tuliseme wazi si kumung'unya maneno

Kama Simon hawakuwa kampuni inayokidhi,serikali ilitakiwa kutafuta kampuni nyingine mbadala na kuikabidhi mradi huo.

Hakuna namna serikali kama serikali inaweza kuendesha miradi ya namna hii. Hakuna! Tusidanganyane! Tutaendelea kutesa tu wananchi ambao wanategemea usafiri wa umma.
Huwezi kumtoa mwekezaji na kuvunja mkataba kama huna vigezo. Mwisho wa siku serikali itashitakiwa na kumlipa fidia mwekezaji kitu ambacho ni hasara kwa mlipa kodi. Dawa ni kumbana mwekezaji atimize wajibu wake, kama akishindwa ndio unapata sababu ya kuufuta mkataba.
 
Huwezi kukomaa kujiimalisha mtu binafsi, badala ya kuimalisha mifumo!utapigwa tu!china/korea kask, watu wanapiga na kuna sheria ya kunyongwa sembuse hapa ambapo kuna pre bargaining!!yeye alidhania kuwa kuzibiti habari ndio soln!!eti hata watu wakapiga wananchi wasijue?!!wakati anaingia madarakani dart ilikuwa inaenda vizuri, akaja akawapiga chini wale selcom waliokuwa wanakatisha tiketi kwa mfumo wa electronic, akawapa tenda ttcl, wakaanza za vishina!!jana anakuja vp kama vile anashangaaa alikuwa hajui!!??pesa hizo zinazopatikana zinakwenda hazina kurudi ni tabu hayo mabasi yatatengenezwa na nini??
Kumbe kuna watu walikuwa wanaomba jamaa atawale milele ili waendelee kupiga pesa
 
Acha kupotosha wewe,

Ukweli ni kwamba huyo marehemu ndiye alikuwa anapiga. Ubabe wake ulikuwa ni zuga tu na uhuni wake. Marehemu amepiga hela ndefu Sana mfano alitumia 1.2 trillion kununua ndege by cash ambapo alilipwa 10% ya hiyo hela ,unafikiri ni sh ngapi?

Yeye alikuwa ni mwizi Namba 1 wa nchi hii.

Usijifanye hujui wakati unajua acha kudemka.
Haya mkuu nimekuelewa
 
Kutokana na mahesabu ya mradi UDART za 2013, gharama ya tiketi ya Mbezi- Kivukoni - Mbezi (round trip) ilipaswa kuwa Tsh 3,000 au Tsh 1,500 kwa safari ya kwenda tu.

Hiyo ndiyo bei inayoweza kulipa ghharama za uwekezaji, gharama za uendeshaji na riba za Benki.

Mradi ulipoanza ulianza kwa Serikali kuingiza Siasa ndipo UDART wakaambiwa wa charge Tsh 1,300 kwa round trip au Tsh 650/= kwa trip ya kwenda tu.

Gharama kubwa sana ya kuendesha UDART iko kwenye Workshop (Karakana). Karakana siyo revenue centre kama yalivyo mabasi, instead yenyewe ni cost centre. Inakula tu na haizalishi.

Hiyo tofauti ya Tsh 3,000 ya kwenye upembuzi yakinifu na ile Tsh 1,300 ya Serikali ambayo imelazimisha ni Tsh 1,700.
Kwa hiyo kila abiria wa Mwendokasi anakokwenda Kariakoo na kurudi anatengeneza hasara ya Tsh 1,700.
Na hapo ndipo inaonekana mradi hauwezi kugomboa magari 70 ambayo yako TPA kuanzia mwaka 2019 yakisubiri yasamehewe Custom duty na Excise tax. Vile vile ndiyo chanzo cha kushindwa kununua magari mapya.

TUSITAFUTE MCHAWI, SERIKALI NDIYO CHANZO CHA KUDORORA KWA UDART
 
wezi waliiba hata kwa nyerere

ngozi laana hii, wallahi Tarrahi
Kwakweli inafikirisha sana. Jinsi Magufuli alivyojipambanua kulinda mali za umma akateua wazalendo kila mahali na sasa haya ndio matokeo kila mradi. Hii ngozi kweli imelaaniwa.
 
Hili jambo mimi nilishindwa kabisa kulielewa, vifaa ambavyo vinaenda kusaidia wananchi serikali inagoma kabisa kuvitoa! Sasa walipata faida gani? Kodi hawajapata, wananchi huduma hawajapata. Si wangeweka special agreements, kila siku 50pc ya revenue iende kulipa kodi, how difficult was that! Watanzania hatujui ni namna gani Mungu ametuokoa na lile jitu.

Na huu ujinga wa BRT Phase 1 ndio umetunyima pesa ya Phase II na III, World Bank waligoma kutoa pesa tena. Maana hii ya kwanza tumechemka.
Mungu katuokoa sana.
 
Hayati aliamini yeye anaweza kila kitu. Hata hii miradi alikuwa anasimamia kutokea Ikulu. Matokeo yake ndio haya katuachia majanga kila mahala.

Sasa kama mimi waziri nipo rais anaruka anaenda kukagua vitu ambavyo vipo chini yangu bila hata kunishirikisha si mwisho naacha tu afuatilie yeye mwenyewe kila kitu.
 
Udart sasa nao wapo kwenye kutumikia karma ya maxcom na karma ya kudhulumu wafanyakazi stahiki zao ikiwemo mafao.

Ukweli hawa watendaji wasio na ujuzi na mambo ya magari ni tatizo sana kwa taasisi nyingi + ukabila uliokuwa umetamalaki kwenye huo mradi ni lazima haya yajitokeze, management iliyoshindwa kuendesha daladala zilizopewa njia bila mshindani kule mnazi mmoja kivukoni na baadae kwenye huu mradi kamwe hawakustahili kupewa hiyo nafasi, maana waliwaletea figisu maxcom wanawaibia pesa wakatolewa wakaanza kukusanya wao Pesa majumbani kwa watu na mifukoni, TTCL Sijui kitu gani kiliwashinda kirejesha mfumo kama ule wa awali wa maxcom, haiingii akilini Mashine za Ku swap kadi na ticket zipo na zimeagizwa kwa Pesa nyingi, cha kuzisimamisha kwa miaka mitatu ni hujuma kubwa sana hii.


Ukirudi kwa wafanyakazi waliomaliza mikataba wengi wao mafao yao na hata michango yao ya kila mwezi haikupelekwa hii pia ni uzembe au kuna watu walikuwa wananufaika na ucheleweshwaji wa kupelekwa kwa michango kwenye mifuko husika.

Miaka mitano sasa ni aibu mradi ule wa mabilioni kushindwa kujiendesha kwa faida na inasikitisha wao mishahara haikosekani ila faida na malipo kwa wastaafu hakuna.

Nitarudi baadae mjukuu wangu analilia simu.
Wivu tu waliona vijana wa kitanzania wanapata sana. Sasa tiketi zinakatwa kutokea nyumbani kama zile za pantoni za wakati ule.
 
Ninayesoma maadishi kama haya ya kwako, moja kwa moja najua we ni bonge la layman. Yaani serikali ikuruhusu kuchezea mali ya umma kwa wizi kwa kuwa tu unalipa hiyo 50% unayodhani ni pesa nyingi sana! Kama unamiliki boda-boda hiyo ni sawa, endelea, lakini siyo mali ya serikali.
Mkuu unadandia treni kwa mbele, hujui post imetoka wapi.
 
Mkuu unadandia treni kwa mbele, hujui post imetoka wapi.
Hizi ni page chache sana kwa ufahamu wangu. Najua sana, na naweza kutabiri thinking yako. Tungekuwa tunaonana usoni, ningeweza ku-judge hata intelligence yako. Mammals' instinct!
 
Kila kizazi kinapojiunga na JF kinajifanya kufundisha wengine, kumbe mambo yanaeleweka siku nyingi. Sijaelewa mtu kama Jidu La Mabambasi anawaza nini kuleta utetezi wa kitoto kiasi hiki. Is this all about his/her thinking? Kama ni urafiki na hao wezi, nalo ni jambo la kujiuliza kwamba unawezaje kuwa mtu wa bei ndogo kiasi hiki hadi kutetea wenye akili mbovu kama hao akina Kisena.
Mkuu mtu aliyeweza kuwekeza hata laki moja na akafanya biashara kwa faida, anakuzidi kiakili kwa mbali sana hata kama una PhD.
Mfanyabiashara anafikiria ALL scenarios to make money.
Nyie watu wa kunyoosha mkono kila mwisho wa mwezi mna mataizo sana.

Tatizo kubwa ni kufikiri kuwa mfanyabiashara yupo hapo ili nyie mliokaa vitini mle na kuota vitambi.
 
Back
Top Bottom