Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Kama mtakumbuka mwaka jana DPP alianza kufuta kesi zote walizofunguliwa watu wakubwa nchini wakiwemo wanachama wa chama Cha mapinduzi. Hadi Sasa pamoja na ubadhirifu wote uliofanyika hakuna hukumu iliyotolewa Kwa Kiongozi yeyote wa chama Cha mapinduzi inayomfanya akae kifungoni. Wakitenda wanaachowa au kulipa faini.
Wakatoa hayo yakifanyika wanachama wa Chadema wameanza kuonja madhila ya HAKI Kwa kuhukumiwa vifungo visivyo na utu. Tulisikia huko Mbeya kijana kahukumiwa maisha jela akidaiwa kuchom nyumba ya mwanaccm
Leo tumesikia huko Lindi wanachama wanne wa Chadema wamehukumiw miaka nane jela. Tuliona Mdude akipishwa njia Hii Hii na mahakama zetu na Juzi tumeshuhudia Mbowe akiambiwa ana kesi ya kujibu.
Tukumbuke Mbeya anatoka spika na Linda anatoka PM na Waziri wa habari na watu Hawa walipita kwenye UCHAGUZI Kwa njia zisizoelezeka. Tunawafunga watu, Wana familia, watoto wanateseka na familia zao zinateseka. Lakini wakati tunafanya haya tunazo tuhuma lukuki nyuma yetu na hakuna wakutugusa. Then tunatoka tunaomba amani na mshikamano.
Huu ukatili unaoendelea nchini kupitia mahakama siyo mzuri kwa kesho yetu. Matajiri na wanafamilia wenye mamlaka na fedha wanatumia fedha kumalizana na mahakama lakini maskini Yao jela.
Ninaumia sana kwamba Tanzania maskini wanaoelekezwa kuishi jela wanaongezeka na mahakimu wanaohusika ni ndugu zetu, mawakili wanaotamka maneno iwe fundisho kwa wengine ni watoto wetu Tena wadogo....hawa watu wakizoeshwa ukatili wa mamlaka huko uzeeni watatufanyaje?