Awamu ya tano hakuna aliye juu ya sheria

Jemmie

JF-Expert Member
Mar 6, 2018
216
285
Moja kati ya mafanikio ya uongozi huu wa Magufuli ni kuwaonyesha Watanzania hakuna aliye juu ya sheria. Awe mbunge, Waziri au kiongozi wa Chama chochote.

Awamu ya nne tulishuhudia Mtu akimwagiwa tindikali na wahusika kuachwa wakiendelea na maisha ya kawaida. Mpaka leo Mh Mbowe anatajwa kuhusika na tukio hilo.

Awamu ya nne pia tukashuhudia mabomu Arusha yaliyoua watu kadhaa. Chanzo cha yote hayo ikiwa siasa chafu za Lema na Mbowe. Hadi awamu ya nne inaondoka madarakani hakuna aliyechukuliwa hatua.

Awamu ya nne hio hio mh Wengwe akafanyiwa zengwe la ajali bado hakuna aliyehusika aliyefikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Maana yake nini? Awamu zilizopita wenye vyeo, pesa na majina makubwa walikuwa juu ya sheria huku wanyonge wakilipa kwa kuumizwa ili tuu wenyewe wasiguswe.

Hali ni tofauti leo, Mh Mbowe anamalizia Mwaka gerezani kwa kuandaa maandamano yaliyoletea kifo cha Akwilina.

Tunasema hii ni hatua na kama Tanzalendo tunapongeza kwa hili. Pia tunapongeza sana wananchi kudharau maigizo.

Mwanzo walidhani watanzania wataandamana Mbowe aachiwe ingawa matokeo yake wanspongeza sana na maafa katika mikutano na mikusanyiko isiyo halali yamepungua.

Tukisema Kazi inafanyika tunamaanisha pamoja na haya.
 
1.Tindu lissu alipigwa lisasi awamu ya tatu
2.sanane alipotea awamu ya kwanza
3.uwanja wa ndege chato umepitishwa na bunge linaloendelea
4.bunge lipo live
5.mikutano ya kisiasa inaendelea vyama vyote ccm bukoba cdm hai .
Ndugu acha ujinga uonevu unaoendelea awamu hii haujawahi kufanyika huko nyuma hata huyo mbowe uliyemtaja aliandamana kudai nini? je ni haki asipewe hadi muda ule?
 
Kuna mmoja ambaye amejichukilia mamlaka ya paymaster general na bunge.
 
Nadhani mleta mada amechanganya kitu.
Japo binafsi kwa mtazamo wangu rais mwenyewe anaonekana kukimzana na sheria.
Matumizi mengi ambayo kimsingi lazima yaidhinishwe na bunge yeye anajipangia mwenyewe.
CAG alitoa taarifa yake kwamba kiasi cha 1.5 trillion matumizi yake hayajulikani lakini yeye ndiye alikuwa wa kwanza kumhoji katika muhadhara athibitishe kama ni kweli. Wakati ni jukumu la bunge kuhoji matumizi hayo wasiyo yatambua.

Kimsingi hivi ni vitisho kwa CAG katika nchi inayofuta misingi ya sheria, bunge huru hakika wangemchukulia hatua kali sana.
Hitimisho kama yeye anakuwa wa kwanza kukinzana na sheria kwa vipi watendaji wake wasizikanyage?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom