Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,891
141,824
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hii ni Serikali ya awamu ya 6 hivyo atakayeshindwa kasi yake ataachwa njiani.

Namshukuru sana Rais Samia kwa kuliweka sawa hili kwani jana watu wengi walinibishia nilipowaambia mimi naamini hii ni awamu ya 6.

Kila zama na kitabu chake.

Maendeleo hayana vyama!
 
Awamu moja ni miaka mitano, sasa yy atarun kwa miaka mitano?
 
Lakini wateule wa rais wapo chini ya kiapo cha agano lililopita.

Kumaanisha hii ni awamu nyingine lazima kuwe na agano kati ya wateule na mteuaji. Agano halithibitiki bila kiapo!
 
Kauli mbiu ya awamu ya sita ni ipi?

kila awamu ina kauli mbiu yake.

mfano Ujamaa na Kujitegemea Nyerere.

Ruksa mzee Mwinyi....

Uwazi na Ukweli Mkapa.

Hari Mpya Kasi mpya Kikwete.

Hapa kazi tu Magufuli
 
Nimemsikia hata mimi,ila inatafakarisha kweli kweli.Maana awamu ni miaka mitano,na Rais wa kila awamu huwa anachaguliwa kwa sanduku la kura.

Mimi nilidhani huyu ni Rais wa sita, ila awamu ni ya tano!Labda tungepata ufafanuzi wa kisheria kutoka kwenye vyombo vyetu vya sheria,maana nilisikia mwanasheria mmoja aliyekuwa amealikwa TBC akisema hii ni awamu ya tano.

Anyway ni ya tano au ya sita sio issue sana,wananchi tunachotaka ni kupiga hatua kimaendeleo.
 
Hapana hii ni awamu ya 5, hii ya sita nani kaichagua na kwa uchaguzi upi? ila raisi ni wa wa 6 labda hukuelewa vizuri.
 
Back
Top Bottom