Rais Samia avunja rekodi ununuzi wa ambulance na magari ya Chanjo

Mtakumbuka awamu ya tano ya Hayati Dk John John Joseph Pombe Magufuli tulifanikiwa kununua jumla ya ambulance 117,awamu hii ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan tumeagiza ambulance brand new 395 || Kaziindelee

" Hakuna kama Samia "

Rais mpole na mnyenyekevu Samia Suluhu Hassan,Rais anayethamini na kulinda Utu na Uhai wa Watanzania wote bila kujali dini, kabila, rangi wala kanda kwa kutumia Economic Stimulus relief fund toka IMF ameagiza zinunuliwe Jumla ya Toyota Land cruiser ambulance mpya 395 pamoja na magari mapya 214 kwaajili ya Chanjo aina zote 15 ikiwemo chanjo ya Corona, Hakika kumbeza Rais Samia nikujitafutia laana za bure kwa Mungu.

Mtakumbuka awamu yetu ya tano katika kutekeleza Ilani ya CCM tulifanikiwa kununua Toyota Land cruiser ambulance mpya 117 na hapa tuendelee kumuenzi na kumwombea pumziko jema Mwanamwema wa Africa Hayati Dk John John Joseph Pombe Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri alizozifanya kwenye sekta hii ya afya nchini.

Kwakuwa Tanzania tuna jumla ya Wilaya 139 na zote zina hospitali za Wilaya baada ya hizi ambulance kufika kila Hospitali ya wilaya itapata ambulance mpya ( brand new) kwaajili ya kunusu roho za Watanzania hawa masikini kwa kuwakimbiza kwenye hospitali za juu yao (referral hospitals).

Kwakuwa Tanzania pia tuna jumla ya Halmashauri 184 ikiwemo Ushetu tulikoshinda kiti cha Ubunge kwa kishindo majuzi kwa hesabu hii ya ambulance 395 kila halmashauri itapata ambulance mpya kwaajili ya kuhudumia ama za Kituoa cha afya ama Zahanati zao kwaajili ya rufaa za wagonjwa wao kwenye hospitali za Wilaya, Watu wa Idara ya afya tunzeni sana mali hizi.

Ambulance hizi 395 ni mara tatu zaidi ya ambulance zote 117 zilizonunuliwa kwa miaka mitano yote ya awamu ya tano ,kwa wenye kumbukumbu nzuri mtakubaliana na mimi kuwa jambo hili halijawahi kutokea katika historia ya nchi hii, " kama kuna mtu wa kumwombea kwa nguvu zote kwa sasa basi ni Rais Samia Suluhu Hassan "

VIVA SAMIA VIVA || VIVA TANZANIA VIVA

Yaani wamewapa mpaka namba! badala ya kutoa hoja mnatoa matangazo!
 
Nimejaa tele mtoto wa mama wa kwanza wa taifa

Mungu amlinde mama yetu

Safari hii umejiunga na genge la wanaotandaza propaganda za mama vs jiwe? Well, hongera kwa kujaribu kutembea juu ya ukuta mwembamba sana. Lakini, tread very carefully on your integrity. CCM si chama “kile kile”, you know.
 
Kwani hiyo safari ingine unayoijua wewe nilikua wapi??

Sijawahi kuwa na kada, ila siku zote ninaamini kwenye taifa kwanza.

Samia Suluhu Hassan ni rais halali wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hilo halipingiki, na ni rais wangu.

Sasa wewe unaponiambia natembea kwenye uzi mwembamba ni kwamba unanitisha kwa lipi?😂😂
Hapo nilichokolichokosea ni kusema Mungu amlinde?? au nimekosea kumwita mama???

Au integrity yako ulitaka niseme Mungu amfanyaje labda???

Kumlinganisha JPM na SSH ni uhuni mwingine na uchonganishi wa maneno ambao hata yeye mama haukubali. Kila mtu ni bora na kila mtu ni tofauti kwa aina yake

Umemjibu vizuri Sana aise,

Hapa Taifa kwanza
 
Miezi sita ya Rais Samia,

Nchi imetulia tuli,
Wawekezaji kama wote
Wahisani kama wote
Wananchi Shangwe kila kona

#KAZIIENDELEE
 
Kwani hiyo safari ingine unayoijua wewe nilikua wapi??

Sijawahi kuwa na kada, ila siku zote ninaamini kwenye taifa kwanza.

Samia Suluhu Hassan ni rais halali wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hilo halipingiki, na ni rais wangu.

Sasa wewe unaponiambia natembea kwenye uzi mwembamba ni kwamba unanitisha kwa lipi?😂😂
Hapo nilichokolichokosea ni kusema Mungu amlinde?? au nimekosea kumwita mama???

Au integrity yako ulitaka niseme Mungu amfanyaje labda???

Kumlinganisha JPM na SSH ni uhuni mwingine na uchonganishi wa maneno ambao hata yeye mama haukubali. Kila mtu ni bora na kila mtu ni tofauti kwa aina yake

Relax. Naamini unajua vyema kuwa mimi sitishi, sichonganishi wala si mhuni, bali mtazamaji mzuri sana. Nilikuwa nakupongeza tu na kukupa ka-advice.

Wasema wewe hujawahi kuwa kada ila muumin wa “taifa kwanza” na mtu wa tofauti kwa aina yako. Pongezi nyingine zaidi kwa hilo. Halina ubishi. Well appreciated. Na mimi ni mtazamaji wa aina yangu.
 
kwani shida nini mkuu?
 
Yamefana sana kabisa, Hongera Rais Samia

Ziara ya Rais Samia Kilimanjaro na Mapokezi Arusha yamefana sana. Watu wanajitokeza kwa wingi kwenye mikutano na pote anasimama, wana hamasa kubwa, wanaonyesha imani kubwa kwa Rais, Upendo mwingi, matumaini na namna anawaongoza, wengi wanakiri na kukubali Mama anafanya Makubwa!
 
Back
Top Bottom