Awamu ya pili ya Operesheni Haki kutikisa tena, itaanzia Kanda ya Pwani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,638
218,073
Ile kampeni ya kuhamasisha upatikanaji wa Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi iliyotikisa Nchini Tanzania ya OPERESHENI HAKI , itaendelea tena baada ya kusimama kwa muda kwenye Kanda ya Pwani na baadaye Zanzibar na Pemba ,

Taarifa hii imetolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh John Mnyika alipokuwa anaongea na vyombo vya habari , ambapo amedai kwamba walilazimika kusitisha operesheni hiyo ambayo tayari imepigwa kwenye mikoa 24 kutokana na kifo cha Mwanachama wao Profesa Baregu , hata hivyo amesifu mafanikio ya operesheni hiyo kote ilikopita na kwamba kwa kadri ya makadirio yao imevuka malengo kwa kiwango cha kutisha .

Chanzo : Mwananchi .
 
Chadema inapenda nchi yetu iwe katika mtindo wa mchaka mchaka kila wakati haya mambo siyo sawa kabisa,vikao vyao vya ndani wafanye bila shida lakini kuwaingiza watu katika mbio mbio kutapunguza ufanisi katika mambo kadhaa wa kadhaa....
 
Watu wanaenda kwenye porojo za kisiasa badala ya kufanya kazi kujiingizia mapato, wakitoka huko wanalalamika maisha magumu. Kweli bongo mi sihami; ujamaa ulitulemaza kabisa!
 
Watu wanaenda kwenye porojo za kisiasa badala ya kufanya kazi kujiingizia mapato, wakitoka huko wanalalamika maisha magumu. Kweli bongo mi sihami; ujamaa ulitulemaza kabisa!
Mbona mikutano ilizuiliwa na watu awakuacha kulalamika maisha magumu au sababu ni upinzani mnaona wanafaidi wakifanya shughuli zao bila bugudha?
 
Back
Top Bottom