Awamu ya pili: Wanafunzi 11,378 wa mwaka wa kwanza wapewa mkopo

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
Maoni BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa orodha ya awamu ya pili yenye jumla ya wanafunzi 11,378 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 35 kwa mwaka wa masomo 2019/20.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru jana ilisema idadi hii ya awamu ya pili inafanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo kufika 42,053 na wamepata mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 148.56. Katika orodha ya awamu ya kwanza iliyotangazwa wiki iliyopita, wanafunzi wa mwaka wa kwanza 30,675 walipata mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 113.5.

Badru alisema katika mwaka wa fedha 2019/2020, serikali imetenga Sh bilioni 450 kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 128,285, kati yao wanafunzi zaidi ya 45,000 watakuwa wa mwaka wa kwanza na wengine 83,285 ni wanafunzi wenye mikopo wanaoendelea na masomo. Mwaka 2018/2019, Sh bilioni 427.5 zilitengwa na kuwanufaisha jumla ya wanafunzi 123,285 wakiwemo wanafunzi 41,285 wa mwaka wa kwanza.

“Tumeboresha sana mifumo yetu na sasa mwanafunzi anaweza kufungua akaunti yake aliyoombea mkopo maarufu kama Student’s Individual Permanent Account (SIPA) na kupata taarifa zake zikiwemo za kiwango cha mkopo alichopata,” alisema Badru. Pamoja na SIPA, Badru alisema majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo katika awamu hii ya pili yanapatikana katika mtandao wa HESLB wa uombaji mkopo (https://olas.heslb.go.tz) na tovuti ya Bodi (www.heslb. go.tz).

“Bodi inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa kwa awamu inayofuata ukiendelea,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo
 
Tunashukuru kwa taarifa
 
Wangapi waliomba...

WangaPi walikuwa na vigezo....

Na waliopewa ni asilimia ngapi ya walioomba na asilimia ngapi ya wenye vigezo??
 
Back
Top Bottom