Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,291
- 2,466
Nimewahi kuweka uzi hapa kuelezea hofu zangu juu ya uongozi huu wa awamu ya tano. Huu hapa. Jana Rais kaongea na jumuiya ya wadau wa chuo kikuu cha dar es salaam wakati akizindua ujenzi wa Maktaba kubwa na ya kisasa. Aliongelea mengi ikiwa ni pamoja na ubora wa elimu itolewayo UDSM, ukanjanja na ukilaza wa vyuo vingine, usafiri wa haraka (U-DART), n.k. Nilichogundua ni kwamba Rais wa sasa akiachiwa kuzungumza atazungumza siku nzima na kisha tukija kuchambua alichozungumza tutabaki kuguna na kutazamana. Tumezoea kuona JK akiwa ni mtu mwenye bashasha mara nyingi wakati akiongea au kumsikiliza mtu lakini jana alikuwa kauchuna muda mwingi. Hata wakati akiongea aliongea akiwa serious zaidi.
Magufuli anasema hataki taasisi nyeti kama UDSM iendeshwe kisiasa na wanafunzi waachane na siasa lakini yeye kapeleka siasa pale na kuuza chai. UDSM sio kama haina mapungufu. Mapungufu mengi yalianzia kwenye uongozi wa makamu mkuu wa chuo wa sasa anayemaliza muda wake. Chuo kilidorora sana. Walimu walikuwa wako wako tu na ndio maana wengi wao walikuwa wakienda kufundisha vyuo vya nje ya UDSM kama Tumaini, OPen University, CBE, IFM, Mzumbe, hadi Mwanza wanaenda kupiga lecture na kurudi! Nawajua sana walimu vinara wa hizo kazi za nje hapo UDSM.
JPM anasema wanafunzi wasijishughulishe na siasa wakati walimu wao wengi wako kwenye siasa. Kina Prof Kitila, Dr. Simon wa Bunge la katiba, Dr. Bana na wengine wengi. Kwa nini walimu wawe wanasiasa halafu wanafunzi wasianze kupractice nadharia zao? Kina Zitto, Shigela, Waitara, n.k ni zao la UDSM. AU anahofia kuwa watakuwa wapinzani?
Rais sasa kaamua kuweka wazi kuwa upinzani wa kisiasa hauna tija na ndio maana kamsifia sana Prof Kitila. Anasahau kuwa yeye ni Rais na kushindwa kuweka uwiano katika mapendo yake. Sasa kahama toka kejeli za kisiasa kahamia kwenye kejeli za kitaaluma. Kiufupi amachafua hali ya hewa ya vyuo vingine nchini. Kwamba havina hadhi ya UDSM. Na hilo suala la UDOM nadhani ndio limemchefua kabisa JK maana aliwekeza nguvu zake nyingi pale kutaka kuona mbadala wa UDSM. Leo watendaji kadhaa kwa ulafi au dhamira au mikakati yao wamefikia uamuzi wa kuweka hiyo taaluma mpya kisha Rais anakuja kuwahukumu hao vijana, mbaya zaidi kwa kuwaita VILAZA wa division 4!
Rais kaumiza nyoyo za watanzania wengi sana. Rais kazungumza kwa upendeleo. Rais hataki kutumia utashi katika kufikiri. Mambo mengine si ya kuzungumza tu tena hadharani, hata kama yana ukweli. Kuna lugha za tafsida. Raisi anaendeleza uonevu kwa dagaa na kuacha makambale yakimea. Wameua hoja za msingi za ufisadi za kina lugumi, escrow, n.k. na kutufanya tuweke mawazo yetu kwenye hoja dhaifu kama hizi.
Nimesoma UDSM. Hivi kwa kiasi gani hawa wahitimu na walimu wa UDSM wameweza kuliwezesha Taifa kufanya maendeleo? Zile faculties (ambazo sasa hivi ni schools) zimewezaje kutoa wahitimu ambao ni wa kupigiwa mfano kwa taifa katika nyanja zao? Aliyesema kipaumbele pale UDSM ni library mpya ni nani? Nini maana ya zile schools? Ile Library kuu kwa muda mrefu imekosa vitabu na majarida yanayokwenda na wakati. Library imejaa vitabu vya miaka ya 1980 ambapo mambo mengi sasa yamebadilikakiuchumi, kisiasa, kisayansi nakiteknplojia.
Tunahitaji kweli mabadiliko lakini yaendane na uhalisia. Si kutukana wengine wasio na uwezo wa kujibu na kuwaacha wababe ambao wanasumbua kila siku. Rais kaa tena na timu yako na uipe nafasi ya kuwasikiliza maana uliwateua, ama uliwakuta. Watanzania jinsi tunavyojuana watakususia mambo mengi kwa kuwa wewe 'unayaweza'. Achia mihimili husika ifanye kazi ipasavyo. Waachie wapinzani wakupe darasa ipasavyo. Juzi nilimsikiliza Mbunge wa Babati mjini, anaitwa Pauline Gekul akimpa somo waziri wa elimu. Niliona waziri akibetua kichwa kukubali huku akiwa anaandika vitu chini na kwa spidi. sasa mnaposhirikiana na na huyo mteule wako ambaye hana mizizi kwenye siasa na kuamua kuwafukuza wapinzani bungeni mnajenga nchi kweli?
Mheshimiwa Rais bado muda unao wa kubadili taswira inayoanza kujijenga. Kama umeshawapa hadi matrafiki mamlaka ya 'kukwapua' matairi ya magari yanayovunja sheria kwenye njia za mwendo kasi, basi usishangae na wananchi wakijichukulia sheria mikononi pale wanapokumbana na uhalifu katika mazingira wanayoishi na kufanya shughuli zao. Tukiulizwa tunajibu tu kuwa "kwani hii gari ilikuja na matairi?"
https://www.jamiiforums.com/threads/rais-magufuli-tafakari-tena-unakoelekea-siko.1023806/