Elections 2010 Awamu ya Kwanza Kampeni ya Dr. Slaa kuelekea Ikulu

hivi huyu anaesema eti kuna watoto ana akili timamu kweli nahisi huyu ni mwana ccm miongoni mwa wale wanaofaidi matunda ya nchi hii jamani mi nasoma udom wananchi dodoma maisha ni magumu si kawaida vitu bei juu hasa baada ya kuingia madarakani huyu mtalii kikwete lakini mijitu mijingamijinga kama hli linalosema kuna watoto linalopoka tu sijui linamaana gani juu ya watanznia ambao wanataka mabadiliko jinga hili jamani watz wapenda mabadiliko kula ccm lakini kura chademaa kwa Dr. Slaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Slaa+Geita.jpg


Dr Slaa anakubalika sana kanda ya Ziwa, lakini mbona naona watoto wapo wengi? Je hawa ni wapiga kura hapo Oct 31?

watoto ni wapiga kura wa kesho na vile vile wanawawakilisha wazazi wao. kwenye matukio mbali mbali si rahisi watoto wakosekane, na unawaona kiurahisi kwa sabau wako mbele kutokana na udogo(sio uchache) wao
 
Mwaka huu ninavyoona hali, lazima Dr. Slaa atashinda. Ili umafia wa CCM uweze kumtangaza JK kuwa ameshinda, wafuatao watapiga kura:-
1. wanajeshi
2. Polisi
3. FFU
4. Wafungwa

Maana kwa hali ya kawaida haiwezekani kufikia hata 20% ya kura zote Tanzania.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Dr. Slaa:playball:

Namba moja mpaka tatu wengi wamepigika kinoma. Mkuu hujapata nafasi ya kuongea nao siku za karbuni, hawana hamu na ugumu wa maisha. Kama watalazimishwa kupiga kura kwa kuonesha, sawa ila kama ni kwa siri itakula kwa CCM
 
Umati wa watu wamehudhuria kumsikiliza Dr slaa ambao anawategemea wamepe kura zao ,wakati wapinzani wake CCM Ushindi wao unatokana na NEC
 
Ujinga wa "electorate" ya Tanzania umejikita zaidi huko vijijini. Ni huko ndipo Dr Slaa inabidi akazanie sana kuelimisha wananchi wenzetu hawa.

Ukiangalia ni rasilimali zote zinazotoka maeneo hayo ya mbali na "administrative capital" ya Dar-es-Salaam ambayo makao makuu ya ofisi zote za wawekezaji na serikali yapo na ndio uratibu wa keki ya taifa unafanywa hapo.

Inajulikana wazi kwamba watu wote wanaoishi Dar ni wale ambao wameridhika na maisha iwe ya raha au ya ubabaishaji na wapo tayari kuharibu utaratibu mzuri wa kidemokrasia wa kuleta mabadiliko.

Hata kama Chadema itashindwa uchaguzi mwaka huu lakini "electorate" itakuwa imeanza kuelimika na baadae tutahitaji serikali ya mseto ili kuweka "balance" na baadae baada ya Chadema au hata chama kingine kushinda uchaguzi wa uraisi, CCM nyo ije ionje raha ya kuwa serikali kivuli bungeni.
 
naona local media inaweza kusaidia CHADEMA na CUF moja wapo ni hii ya kuweka blog za wagombea kama dira yetu blog post na kuweka khabari zao kila wanapofikia kuhutubia wananchi DIRA YETU
tujifunze kwa wenzetu Kenya muda mchache tu uliopita nimeweza kuona picha ya slaaa tayari kweney blog mbali mbali na jamii forum, najua Vyama hivi havina pesa za kuwahonga kina michuzi na waandishi wengine lakini vyama hivi vinaweza kuwa n Blog moja tu ya kuweza kuwaelimisha maelfu ya watanzania ni ukweli pia watanzania wengi wanatumia internet siku hizi hata kwa hiyo wanachadema na wana CUF changamkeni musidharau technology.
 
watoto ni wapiga kura wa kesho na vile vile wanawawakilisha wazazi wao. kwenye matukio mbali mbali si rahisi watoto wakosekane, na unawaona kiurahisi kwa sabau wako mbele kutokana na udogo(sio uchache) wao


ukiweka percentage ni ngapi ni watoto hapo just count watoto wangapi chini wa watu wote hapo times 100.

Kisha niambie mkutano gani wa kampeni hizi ambao haukuwa na watoto.
 
Nimeona kitu kimoja tofauti ktk mikutano ya CCM na Chadema. Ukitazama ile ya CCM viti vya mbele vyote pamoja na safu nyingi karibu na mgombea huchukuliwa na wana CCM tena wengi hupewa viti vya kukalia hali wananchi wapiga kura huachwa nyuma wamesimama mbali na jukwaa. Ukija Chadema utakuta wananchi ndio wanakuwa karibu na jukwaa kwa umbali usiozidi mita 10..

Pili, nimeona kila viongozi wa CCM wanapohutubia husiamama nyuma ya mic iliyo still hali Chadema mgombea wake huzunguka ktk jukwaa na kuwafuta wananchi karibu kuonyesha hali halisi kimwili kwa kila analozungumza (body language).

Tatu, Chadema imekuwa ikizungumzia zaidi hali ya matatizo ya wananchi na jinsi gani watakavyo weza kuyaondoa wakati CCM imekuwa ikitoa ahadi ambazo sii lazima ziwe kero za wananchi. Kushindwa kuelewa kero za wananchi na kuwahakikishiqa kuondoka kwa kero hizo badala yake kuwapa ahadi za utajiri zaidi kabla hujazikabiri kero zao ni hadithi ambayo sii lahisi kuuzika. CCM kwa kila hali nan mali ni lazima wazungumzie Ufisadi na jinsi gani wataweza kuukomesha kisera.. Ni mikakati gani imewekwa kuhakikisha hali iliyotokea miaka 10 iliyopita haiwezi kutokea tena...Lakini kuendelea kukataa lawama ambazo zina ushahidi tosha kwa wananchi na hasa wa wa vijijini ambao wameona jinsi viongozi wao walivyoweza kujineemesha na serikali hii ni vigumu sana kuwashawishi tofauti...

Hadi sasa hivi mimi nadhani Chadema wana score points nyingi sana dhidi ya CCM isipokuwa tu Chadema walipuuza sana kutoweka wagombea sehemu muhimu sanavijijini toka serikali za mitaa, kata (madiwani) na hata majimbo kwani ushindi dhidi ya CCM unahitaji sana nguvu kubwa kutoka chini (vijijini) ambako bado wananchi hawaelewi kama kuna maendeleo zaidi ya hayo waliyokuwa nayo...
 
Mkandara,
CCM hawawezi kuzungumzia ufisadi na jinsi ya kuutokomeza kwa sababu watakuwa kama wanajikata mguu. Wameingia mamlakani kwa ufisadi, wanashinda kura kwa ufisadi, wanaogombea ni ufisadi wannabees. Ufisadi umekuwa sehemu ya utamaduni wao. Kuna rafiki yangu mmoja karudi juzi kutoka Ukerewe ananiambia yule mbunge wetu wa CCM alikuwa anatumia vilio na mazishi kugawa kanga kwa akina mama. Sasa hawa unategemea kuwa wataweka sera za kutokomeza ufisadi? No way.
 
Genakai . . . . naona kama sasa hivi ni kama kunapambazuka, asubuhi bado wala mchana . . . .

Duru za habari zilisema mwanzo kuwa Dr. Slaa ana mabomu kama 9 hivi . . . sina uhakika kama ameanza kuyatumia . . .

Kazi kweli kweli.

Kwa sababu kampeni ni kama mbio za marathon - pale mwisho mwisho ndipo ataongeza kasi na kuwapita wengine, atawanyong'onyeza kwa hayo mabomu - na mabomu ya huyu Dr. Wilbroad ni yale ya aina ya 'cluster' yaani yakiripuka yanasambaa kama vibomu vidogo ambavyo navyo ulipuka!!
 
Sasa CCM ndo wanaona umuhimu wa Nyerere.
Mbona Kingunge hapandi jukwaani kuwasaidia kama anavyowasaidia kuwafokea waandishi wa habari?
 
Tz si unajua ni jamvi la wageni whoever comes is accepted and worse enough he has the nerve to become a leader regardless of his origin
 
Back
Top Bottom